30.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

TEF, DCPC walaani udhalilishaji dhidi ya mwandishi wa ITV

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania (TEF) limelaani udhalilishwaji unaofanywa na baadhi ya viongozi nchini dhidi ya waandishi wa habari na kuwataka kutambua na kuheshimu umuhimu wa vyombo vya habari.

TEF kwa kushirikiana na Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) limetoa tamko kulaani udhalilishwaji uliofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi dhidi ya Mwandishi wa ITV, Richard Steven.

Desemba 2, mwaka huu Steven alimpigia simu mkurugenzi huyo kuomba ufafanuzi baada ya wananchi wa Mtaa wa Magogoni uliopo Manispaa ya Temeke kuzuia ujenzi wa Shule ya Sekondari Lumo lakini Mwakabibi alimshambulia kwa kauli zilizojaa kejeli na dhihaka kisha akakata simu.

Akizungumza leo Desemba 4 katika ofisi za DCPC, Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, amewataka waandishi washikamane na waendelee kwenda Temeke kutafuta habari.

“Dosari dhidi ya waandishi wa habari ni ishara ya kutostarabika, sina hakika sana lakini unaweza kukuta wakurugenzi wa namna hii ndiyo halmashauri zao zinapata hati chafu. Viongozi na Watanzania kwa ujumla watambue na kuthamini umuhimu wa vyombo vya habari,” amesema Balile.

Naye, Mwenyekiti wa DCPC, Irene Mark, amesema kitendo kilichofanywa na mkurugenzi huyo ni kinyume na kifungu cha 7 cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kinachompa mwandishi mamlaka ya kukusanya, kuchakata na kuchapisha habari.

“Sisi tunachukulia dhihaka za Mkurugenzi Mwakabibi kuwa ni udhalilishaji mkubwa si tu kwa Mwandishi, Richard Steven peke yake bali kwa tasnia nzima ya habari nchini. Tunalaani kitendo hiki na tunamtaka Mwakabibi kumuomba radhi mwandishi huyu na tasnia ya habari kwa ujumla,” amesema Mark.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles