21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani watakiwa kusikiliza kero

Na Elizabeth Kilindi, Njombe.

Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, Joseph Kamonga (CCM) ametoa rai kwa madiwani wateule kupitia Chama hicho, kuweka mkakati wa pamoja wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua na ambazo zipo nje ya uwezo wao wazipeleke sehemu husika.

Rai hiyo imetolewa juzi wenye mkutano wa uchaguzi ndani ya chama pamoja na mafunzo kwa madiwani ambapo alisema kusikiliza kero za wananchi si kazi ya mkuu wa wilaya na mkurugenzi pekee.

“Ninawaomba sana tushirikiane na tuwe pamoja ili tuweze kutatua kero za wananchi katika jimbo letu la Ludewa kwani changamoto zao tunazifahamu na sio tuwaachie madc na maded tutimize wajibu wetu”alisema Kamonga.

Kamonga alisema kuwa, Rais Dk. John Magufuli ameelekeza kuwa viongozi wa kisiasa wanapaswa kufahamu kuwa shughuli ya kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi nao zinawahusu pia.

Pia aliwataka madiwani hao pindi wanapopanga ratiba za kwenda kusikiliza kero za wananchi katika jimbo hilo wasisite kumshirikisha ili kwa pamoja waweze kutatua kero za wananchi katika jimbo hilo.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere, aliwapongeza madiwani hao wateule kwa ushindi walioupata na kukiwezesha chama hicho kushinda kwa kishindo ka kupata kura za urais zaidi ya asilimia 88 katika wilaya hiyo.

Aliwataka madiwani hao kumchagua Mwenyekiti atakayesimamia Halmashauri hiyo vizuri kwa maslahi ya wananchi ili wapate maendeleo na kuacha kuchagua kiongozi kwasababu wamepatiwa kitu fulani.

“Hapa tunamchagua mtu tunayefikiri kwamba atashirikiana vizuri na chama hiki, viongozi wa halmashauri akiwemo mkurugenzi, wakuu wa idara pamoja na watu walio chini yake huyo hapatikani kwa hela bali kwa uwezo”alisema Tsere.

Katika uchaguzi huo wa ndani ya chama uliokuwa na wajumbe 32 akiwemo mbunge Kamonga, walipiga kura na kumchagua, Wise Mgina kuwa Mwenyekiti wa kamati ya madiwani wa chama hicho kwa kura 19 akimshinda aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Haule Edward aliyepata kura 13.

Hata hivyo nafasi ya makamu mwenyekiti iliyokuwa ikigombewa na mtu mmoja Edger Mpambalioto na alipigiwa kura za ndiyo na hapana ambapo kura za ndiyo alipata 18 na hapana kura 14.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles