30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

DC Waging’ombe ataka michango ujenzi wa bweni

Na Elizabeth Kilindi, Njombe.

Watendaji wa Kata, Kijiji na Bodi shule ya Sekondari Igima wametakiwa kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa michango ya ujenzi wa bweni jipya la wavulana katika shule hiyo lililoungua moto Septemba, mwaka huu.

Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe, Lauter Kanoni wakati akipokea mifuko 250 ya saruji kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bweni hilo.

Kanoni alisema kulingana na makubaliano kila mwananchi anapaswa kutoa mchango wa kiasi chaSh 10,000 hivyo yatekelezwe kabla ya hatua kali za kisheria kuchukuliwa.

“Naelekeza mtendaji wa kijiji, kata na bodi ya shule vile viwango ambavyo tulipangiwa kila anayestahili kuchangia afanye hivyo na ikipendeza kabla ya krismasi jengo liwe limesimama na kupauliwa libakie vitu vidogo vidogo,”alisema Kanoni.

Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Edes Lukoa alisema kutokana na changamoto ya kupanda kwa saruji katika kipindi kilichopita kiliwalazimu kusimamisha ujenzi wa bweni hilo lakini kwa sasa ujenzi unaendelea.

Lukoa alisema hadi kukamilika kwa jengo hilo linatarajia kutumia zaidi ya shilingi milioni 75 fedha ambazo ni michango ya serikali,wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.

“Tuliomba bati pamoja na saruji ambapo wenzetu shirika la nyumba walipokea ombi letu hili na kwa kiasi kikubwa wametusaidia kwani tuliomba mifuko 200 ya saruji lakini wametupatia mifuko 250,’alisema Lukoa.

Nae, Meneja wa NHC Nyanda za Juu Kusini, Said Bungara alisema baada ya kupewa taarifa hiyo ya kuungua kwa bweni hilo kama wadau waliona ni muhimu kuchangia nusu ya mifuko ya saruji ili wanafunzi waendelee kuishi katika mazingira salama.

“Tunaunga mkono jitihada za serikali yetu ya awamu ya tano hivyo tulivyosikia kuna jambo la kuchangia watoto wetu ukizingatia elimu ndiyo msingi wa maisha tukasema tujitoe kadri tuwezavyo,” alisema Bungara.

Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Igima, Mika Mbembati alisema hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika ujenzi wa bweni hilo zinawapa matumaini ya usalama wa maisha yao pamoja na masomo.

“Tulipopata janga hili wengi walishindwa kusoma hasa sisi wavulana kwakuwa vitu vyao vinavyohusiana na kusoma viliungua,”alisema Mbembati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles