24.8 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Daktari aeleza madhara ya joto

Na Aveline Kitomary, Dar es Salaam

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Tatizo Wanne ameeleza madhara ya joto kwa afya na hatua zinazotakiwa kuchukulia.

Katika mahojiano maalum na MtanzaniaDigital jijini Dar es Salaam, Dk Wanne amesema madhara ya joto ni kutokwa na jasho jingi hali inayosababisha kupoteza maji mengi mwilini.

“Kwa kawaida mwili unakuwa na kiwago cha joto ambacho kinasaidia kufanya kazi mbalimbali. Joto linapoongezeka kutokana mazingira kama jua kuwa kali au mabadiliko tabia ya nchi kunakuwa na athari mbalimbali katika mwili kwani kunapokuwa na joto mtu anatoka jasho jingi sana hivyo mtu hulazimika kunywa maji mengi ilikuweza kurejesha kiwango kilichopotea,”ameeleza Dk. Wanne.

Amesema kuwa maji yanapopotea shinikizo la damu (presha) inaweza kushuka hivyo hata kiwango cha damu kinachozunguka mwilini kwenye viungo kama moyo inapungua.

Dk. Wanne ameshauri watu kunywa maji kipindi cha joto kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya.

“Kwa afya nashauri kunywa maji kama inavyoelekezwa na wataalamu wa afya hii inategemea na uzito na magonjwa ambayo mtu anayo ni bora kusikiliza wataalamu wa afya kuhusu kiwago sahihi cha unywaji maji,”ameshauri.

Dk. Wanne anabainisha hayo katika kipindi ambacho tayari Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imetaarifu juu ya kuwapo kwa kipindi cha joto kwa baadhi ya maeneo hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles