33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

“Tumieni mamlaka kupata taarifa sahihi”-Tantrade

Na Safina Sarwatt, Rombo

Watanzania wanaofanya biashara mipakani wametakiwa kuzitumia Mamlaka zilizopo kupata taarifa sahihi za biashara wanazozifanya ili kuondoa vikwazo vinavyojitokeza kwenye mipaka hiyo.

Akizungumza leo Jumatatu, Desemba 14, katika Kituo cha Pamoja cha Jumuiya ya Afrika Mashariki cha Holili, Meneja Masoko wa ndani kutoka Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Getrude Ngweshemi amesema wafanyabiashara wengi wamekuwa wabunifu wa kutafuta biashara kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine lakini changamoto kwao imekuwa ni namna ya kupata taarifa za biashara na taratibu jambo ambalo imekuwa kikwazo kikubwa kwao.

“Watanzania ambao ni wafanyabiashara, wanaofanya biashara mipakani wengi hawajui taratibu za kufanya biashara zao, unamakuta mfanyabiashara wa kitanzania anakwenda kuchukua mafuta ya kula Kenya na kuyaleta hapa nchini, na pindi anapoyafikisha anayauza kwa bei ya chini hali ambayo inachangia kuua soko la ndani la mafuta,”amesema Mwashen.

Kwa upande wake Afisa Mwandamizi wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Faith Gugu amewataka wananchi wanaoishi mipakani kutumia mipaka hiyo kufanya biashara na kujitajirisha kwa kufuata sheria, na kwamba jukumu la serikali ni kuhakikisha wananchi wananufaika na si kuonekana kuwa kikwazo.

Amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu kuhusiana na taarifa mbalimbali za kikodi na ambazo sio za kikodi kwenye mipaka hivyo ni lazima sekta binafsi na serikali kuzijua changamoto wanazokumbana nazo wafanyabiashara na kuzifanyia kazi ili wananchi wanufaike na fursa zilizopo katika mazingira yao.

Gugu amesema changamoto waliyoibaini katika mpaka wa Holili, wafanyabiashara ambao ni Watanzania wamekuwa wakichangamkia fursa za mipakani kwa kwenda kununua bidhaa nchi jirani ya Kenya na kuja kuziuza hapa nchini hali ambayo inachangia kuwanufaisha majirani na kuua soko la ndani.

“Tumeona umuhimu wa kufanya ziara hii kwa upande wa Kanda ya Kaskazini kwani ni moja ya mipaka ambayo inatumika Sana na wafanyabiashara wadogowadogo, ambao wengi ni wanawake ambao wanafanya biashara kwenye mipaka hii ya Tanzania na Kenya,” amesema Gugu.

Mwakilishi wa Ushiroba wa Kati, Ally Kakomile amesema lengo la ziara hiyo ni kutoa elimu, jambo ambalo litasaidia wafanyabiashara kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa kupitia bandarini.

Naye, Meneja msaidizi wa Forodha Mkoa wa Kilimanjaro (TRA), Edwin Iwato amesema baadhi ya wafanyabiashara wengi hawana taarifa za kutosha kutumia fursa mbalimbali zilizopo katika maeneo ya mipakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles