Dabo kurekodi na Wajamaika

Dabo 2

MKALI wa muziki wa dancehall nchini, Laban Mbibo ‘Dabo’, ameweka wazi kwamba yupo mbioni kurekodi na wasanii mbalimbali wa muziki huo wakiwemo wa kutoka nchini Jamaika.

Dabo alisema albamu yake atakayoitoa mwaka huu itakuwa na nyimbo nyingi alizoimba mwenyewe isipokuwa moja tu ndiyo ameimba na msanii wa Bongo Fleva, Mwasiti.

“Nikishaitoa albamu hii itakayokuwa na jumla ya nyimbo 12, itakayofuata kwa ajili ya mwakani itakuwa tena na nyimbo 12 nitashirikisha wasanii wengi kutoka nje wakiwemo kutoka Jamaika, Uganda, Malawi na Bukinafaso,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here