23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake washiriki mafunzo ya kuogelea

kuogelea

Na WINFRIDA NGONYANI -DAR ES SALAAM

WANAWAKE zaidi ya 100 juzi walishiriki mafunzo maalumu ya mchezo wa kuogelea yaliyojulikana kama ‘MV Mama’ ambayo yalifanyika katika fukwe za klabu ya Navy zilizopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Mafunzo hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya San Lam Insurance, yaliandaliwa kwa lengo la kuwafundisha wanawake mbinu za kujiokoa katika majanga yatokanayo na maji kwa kuwa wanawake wengi na watoto huathirika ajali zinapotokea.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa klabu ya kuogelea ya Marine Tanzania (TMSC), Geofrey Kimimba, alisema washiriki wamepata fursa ya kujifunza kanuni za usalama majini, uokoaji, huduma ya kwanza kwa aliyeokolewa na matumizi ya vifaa mbalimbali.

“Programu ya mafunzo ya ‘MV Mama’ itakuwa endelevu kwa kuwa inalenga kuleta mabadiliko kwa jamii hasa upande wa kuogelea, tutaendesha mafunzo ya kujiokoa na kufundisha mchezo wa kuogelea kwa rika zote,” alisema.

Mafunzo hayo yanatolewa bure na klabu ya TMSC yakihusisha wanawake wenye umri zaidi ya miaka 18 wasiojua kuogelea ambayo hufanyika kila mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles