
ADAM MKWEPU NA MITANDAO,
MWAKA 2002, mashabiki wa timu ya Manchester United walihamaki na kudai kocha wa zamani wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson hawezi kuendelea kuifundisha timu hiyo kwa kuwa hakuwa na jipya.
Mwandishi wa gazeti la Sunday Times la Uingereza, Hugh Mcllvanney anasema kwamba baadae mashabiki hao walisikika wakisema kwamba kocha huyo alikuwa na bahati ya kuendelea na kibarua hicho.
Mcllvanney anaongezea kuwa labda mashabiki hao walitakiwa kuhakikisha kocha huyo anazikwa kabla ya kusherekea msiba wake kwa kuwa Sir Ferguson anaamini anaweza hasife katika kizazi chake.
Huo mstari wa mwisho wa Mcllvanney bado unaendelea kuzivuruga akili za mashabiki hao si kwamba unapatikana katika film ya Leonardo DiCaprio aliyechukuwa tuzo ya mwigizaji bora anayefanana na Brian Kilcline.
Sababu kubwa ni Cristiano Ronaldo amekuwa katika vichwa vyao mithiri ya film ya ‘Revenant’ ndani ya michuano ya Euro 2016.
Katika hatua ya makundi nyota huyo alizidisha mzuka wa Iceland na kitendo chake cha kukosa penalti katika mchezo dhidi ya Austria,kilikosolewa na kumfanya afanye mambo makubwa kuliko ilivyotarajiwa.
Kulikuwa na maswali machache yasiyostahili yakimaanisha huenda kiwango cha Ronaldo kimekwisha ingawa ni haki kwa kila binadamu anayefikiri sawasawa.
Ni kweli kwamba mashabiki wa soka hawawezi kunyamaza kuelezea mapungufu wanayoyaona kutoka kwa wachezaji hodari lakini Ronaldo anaamini ataendelea kuishi milele katika vichwa vya kizazi chake baada ya michuano ya Euro 2016.
Kukosolewa na kunyooshewa kidole ni moja ya changamoto zilizomjenga nyota huyo katika michuano ya Euro 2016 na kuanza kufanya vizuri licha ya awali kuonekana hana bahati.
Ronaldo anaamini katika ubora wake wa kipekee, ingawa bado anajiuliza kama atakuja kupata nafasi nyingine ya kushinda michuano mikubwa kama hiyo akiwa nahodha wa Ureno.
Kila akifikiria umri wake hana jinsi, kwani akiwa na umri wa miaka 19 alishuhudia timu yake ikifungwa dhidi ya Ugiriki katika fainali ya Euro 2004 na baada ya kukosa nafasi ya kutwaa taji hilo alijikuta akidondosha chozi la uzuni na uchungu kwa taifa lake.
Tangu hapo amefanikiwa kucheza nusu fainali mbili ikiwamo ya Kombe la Dunia mwaka 2006 na Euro mwaka 2012 kabla fainali ya jana.
Lakini katika kampeni ya kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia ndani ya miaka miliwi iliyopita, Ureno ilionekana kupotea katika ulimwengu wa soka Duniani.
Ureno imeingia Euro 2016 ikiwa na mchezaji wa nafasi ya beki mwenye umri wa miaka 38, hiyo ilikuwa ikimaanisha haikuwa na beki wala winga wa kueleweka huku mfumo waliokuwa wakicheza ulionekana kama uyoga kutokana ulivyokuwa wa kubahatisha.
Timu nzima ilikuwa ikitegemea uwezo wa Ronaldo na ukweli juu ya hilo ulionekana katika mchezo dhidi ya Wales na Hungary.
Ushawishi wa nyota huyo ndiyo uliijenga timu hiyo, kadri muda ulivyozidi kuyoyoma kama ilivyotokea kwa Diego Maradona katika fainali ya Kombe la Dunaia nchini Mexico, mwaka 1986 ambapo alifanikiwa kufunga mabao matatu na kutengeza matatu.
Michuano ya Euro 2016 iliyomalizika jana ilimpa nafasi Ronaldo ya kutengeneza CV kwa hatua aliyofikia kwa kuiongoza vena timu yake ya taifa ya Ureno.
Wakati walipotoka sare ya bao 1-1 katika hatua ya makundi ilifahamika bao dhidi ya Austria lingeweza kuwaondoa kwenye michuano hiyo.
Ureno hawakukata tamaa na kujikuta wakibadilika kila kitu katika timu yao baada ya kuanza kushinda kwa ushambuliaji wa kushitukiza.
Kusuasua kwao kuliwafanya kujiuliza wakiwa nafasi ya tatu katika kundi lao ambapo safari yao ilianza kuwa hadithi ya kipekee kwa kuanza kuzifunga Croatia. Poland na Wales.
Kufanikiwa kwa Ureno na kufanikiwa kwa Ronaldo kutimiza majukumu yake ipasavyo uwanjani kama nahodha wa timu hiyo, thamani yake inaweza kupanda na kuwa zaidi ya Lionel Messi na Zinedine Zidan ambaye amekuwa mchezaji bora kuwahi kutoka tangu enzi za Maradona.
Ubora wa Ronaldo unachangiwa na vitu vingi hivyo kwa wanaomchukia haimaanishi wataendelea kuwa katika hali hiyo kila wakati, kutokana na mafanikio yake nyota huyo ataendelea kuwa revenant ambayo inaelezea kwamba mtu akifanya makubwa jina lake litaendelea kuishi kutokana na kile ambacho amekifanya.