24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Nani sahihi kati ya TFF na Muro?

Jerry Muro
Jerry Muro

NA BADI MCHOMOLO (+255714107464),

Wiki iliopita, Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF), liliingia kwenye mgogoro na ofisa habari wa klabu ya Yanga, Jerry Muro na shirikisho hilo kutoa maamuzi ya kumfungia msemaji huyo wa Yanga.

Shirikisho lilitoa tamko la kumfungia msemaji huyo kwa mwaka mmoja kutojihusisha na masuala ya soka na kutakiwa kulipa faini ya kiasi cha fedha Sh milion 3.

Sababu za kufungiwa kwa Muro ni inadaiwa kwamba amekuwa akitoa lugha ya kashfa kwa shirikisho hilo, wakati kosa la pili likuwa ni kukiuka maagizo ya kamati ya nidhamu ambapo mwaka jana ilikaa na kumtaka kiongozi huyo kulipa faini ya Milioni tano lakini hakulipa.

Lakini katika kashfa hii ya kutoa lugha chafu kwa shirikisho, jambo hilo lilionekana sio kosa kulingana na kanuni ambayo kamati iliitumia ya 73, pamoja na kanuni ndogo ya 5.

Kosa lingine ambalo linamkumba Muro ni kuchochea vurugu Juni 26 mwaka huu ambapo kiongozi huyo aliwataka mashabiki wa Yanga kukaa pande zote za uwanja wa Taifa katika mchezo wa Kombe la shirikisho dhidi ya TP Mazembe.

Kwa mujibu wa kanuni namba 73 na kanuni ndogo namba 4, ni kosa na adhabu yake ni kufungiwa kutojihusisha na masuala ya soka sio chini ya mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa kanuni namba 73 na kanuni ndogo ya 8 kwa makosa hayo mawili, kiongozi huyo anastahili adhabu ya kufungiwa kutojihusisha masuala ya soka kwa muda husiopungua mwaka mmoja.

Hata hivyo Muro anawashangaa TFF kutoa tamko hilo huku akidai shirikisho hilo halina mamlaka ya kumzuia kiongozi huyo kutojihusisha na masuala ya soka kwa kipindi chochote.

Tangu tamko hilo litoke Muro amezidi kuongea kwa kujiamini huku akiwashangaa viongozi wa shirikisho hilo kutokana na maamuzi yao ambayo kwake anaona sio sahihi.

Muro amedai kwamba watu pekee ambao wanaweza kutoa tamko hilo ni viongozi wake wa Yanga ambao wamempa mkataba wa kuitumikia timu hiyo, na sio watu wengine wowote.

Ukweli uko wapi juu ya mamlaka ya kutoa hukumu kama hii? Inawezekana Muro yuko sahihi au TFF, na kama Muro yuko sahihi basi alitakiwa kuchukuliwa hatua ya shirikisho kutokana na kuchochea vurugu kwenye mchezo wao dhidi ya TP Mazembe ambapo kulikuwa na uharibifu mkubwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Hivyo wanaweza kumlipisha faini kutokana na baadhi ya makosa yake na sio kumfungia kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja wakati wao sio wahajiri wake, lakini kama kweli TFF ina mamlaka hayo basi lazima Muro achukuliwe hatua.

Muro amekuwa na maneno ambayo hayana maana yoyote kwenye maendeleo ya soka kikubwa anachokifanya ni kusherehesha kwa mashabiki wake.

Hadi sasa tunasubili kuona ukweli uko wapi kati ya Muro na TFF kwa kuwa kila mmoja anadai yupo sahihi, hata klabu ya Yanga yenyewe imedai kushangaa na kauli ya TFF juu ya hukumu hiyo kwa Muro na kudai kwamba TFF hawana mamlaka hayo.

Jambo la kushangaza ni kwamba kuna taarifa zilidai kwamba kiungozi huyo anaweza kukata rufaa juu ya hukumu yake na kupinga maamuzi ya kamati hiyo kama hajaridhika nayo.

Hapo napo wanaweza kumpa Muro jambo la kusema kwa kuwa hadi anafikia hatua ya kusimama mbele ya vyombo vya habari na kuishangaa TFF ina maana kwamba hajaridhika na maamuzi hayo na hayupo tayari kulipa faini wala kutumikia kifungo hicho.

TFF walitakuwa kutoa tamko ambalo limesimama kama kweli wana uhakika na kile ambacho wanakifanya na sio kuyumbishwa au kumpa mtu namna ya kufanya wakati kweli ana makosa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles