22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

CRDB yasisitiza ‘Hati fungani ya kijani’ kuokoa mazingira

Na Yohana Shida, Geita

BENKI ya CRDB imejipanga kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kulinda mazingira kupitia mauzo ya hati fungani ya kijani ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Meneja Biashara wa CRDB Kanda ya Magharibi, Anselm Mwenda amesema hayo hivi karibuni katika viwanja vya Maonyesho ya Teknolojia ya Madini mjini Geita.

Alisema kupitia hati fungani ya kijani wadau wanaruhusiwa kuwekeza kuanzia Shilingi laki tano na kuendelea na kupata faida ya gawio ya asilimia 10.25 ambayo ndiyo faida kubwa zaidi ya gawio kwa sasa.

“Mradi wa hati fungani ya kijani zimeletwa kwa ajili ya kuboresha mazingira na kufadhili miradi ile ambayo inatunanza mazingira ambapo tumeandaa dola milioni 300 sawa na milioni 780 ambayo itaelekezwa huko.

“Huu siyo mradi wa kwanza wa mazingira, mwaka 2019 CRDB iliingia makubaliano na mfuko wa dunia wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo ilianza kukopesha pesa kwa miradi rafiki kwa mazingira.

“Kwa mwaka jana peke yake tumekopesha mkopo wa jumla ya Sh bilioni 1.6 ambapo katika fedha hizi Sh bilioni 1.5 zimeelekezwa kwenye miradi ya misitu sawa na asilimia 95 ya fedha zote za miradi,” amesema Anselm.

Anselm amebainisha pia wamekuja na programu ya pendezesha Tanzania ambayo inafanyika nchi nzima kwa ajili ya upandaji, na kwa kanda ya magharibi kwa Mwaka jana walianza na Shinyanga kwa kupanda miti 3,000.

“Lakini kwa mwaka huu tumeanza hiyo program kwa mkoa wa Geita, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita ambapo tumepanda miti 200 na tunasubiri miundombinu ikawe sawa tupande miti mingi zaidi.

“Benki ya CRDB ipo katika huo mpango wa kuhakikisha inaboresha mazingira na mpango huu ni wa nchi nzima na tumeanza na matawi yetu ya kanda ya magharibi lakini tunaenda na hii programu nchi nzima,” amesema.

Waziri wa Muuungano na Mazingira, Dk. Suleiman Jaffo amewapongeza CRDB kwa miradi hiyo kwa kufungamanisha huduma na utunzaji wa mazingira na kusaidia kukabili mabadiliko ya tabia ya nchi.

Ameahidi serikali inaendelea kuunga mkono taasisi zoet zinazotekeleza miradi ya utunzaji wa mazingira huku akiwataka CRDB kumpatia mpango kazi wa miradi yao ili aweze kuipitia na kuona namna ya kuiongezea nguvu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles