27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

CRDB yasaini makubaliano kushirikiana na Care International

*Lengo ni kuwawezesha wanawake kupata mafunzo na mitaji kupitia IMBEJU

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Benki ya CRDB imesaini makubaliano ya kushirikiana na Shirika la Care International kuwawezesha wanawake kupata mafunzo na mtaji wezeshi kupitia program ya IMBEJU.

Akizungumza kwenye hafla ya utijia saini makubaliano hayo iliyofanyika Mei 5, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Mwambapa ameishukuru Care International kwa utayari wao wa kushirikiana na CRDB Bank Foundation katika program hiyo.

Aidha, Tully amewakaribisha wabia wengine kushiriki katika programu hiyo ili kuwafikia wanawake wengi zaidi nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Care International, Prudence Masako ameishukuru CRDB Bank Foundation kwa fursa ya kushirikiana kuwawezesha wanawake kupitia programu ya IMBEJU.

Prudence amesema ushirikiano huo utakwenda kusaidia juhudi zao za kukabiliana na umasikini.

Program ya IMBEJU ilizinduliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Machi 12 mwaka huu na kufungua dirisha la maombi ambapo kwa upande wa biashara bunifu za vijana maombi 706 yamepokelewa na 196 kukidhi vigezo vya kuendelea na hatua ya pili.

Tully amesema dirisha la maombi kwa upande wa wanawake wafanyabiashara bado lipo wazi na kuwataka wanawake kuendelea kuchangamkia fursa zinazotolewa kupitia program ya IMBEJU.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,414FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles