27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 12, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenge wazindua kituo cha kisasa Mafinga

Na Raymond Minja, Mafinga

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdala Shaibu Kaim ameweka jiwe la msingi katika kituo cha mafutu cha Njombe Filling Tastion (NFS) cha mjini Mafinga kitakachogharimu Sh milioni 850,000,000.

Kukamilika kwa kituo hicho cha mafuta ambacho kitatoa huduma mbalimbali ikiwemo vilainishi vya Magari kitatoa ajira zaidi ya watu 30 ambo wanufaika wake ni wakazi wa Mafinga.

Akiweka jiwe la msingi katika kituo hicho kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdala Shaibu Kaima amepongeza mwekezaji wa kituo hicho, James Mwinuka kwa kuwekeza katika mji huo wa kibishara kwani kituo hicho kitasaidia kukuza uchumi wa watu wa Mafinga.

Kaim amesema kuwa Serekali imepanua wigo wa wekezaji nchini ili kuendelea kufungua fursa za kibiashara nchini jambo ambalo pia ni faida kwa serekali kwani itakuwa ikiongeza mapato yake.

“Niwapongeze sana kwa uwekezajii huu mkubwa, mbio za mwenge zimeridhishwa na mradi pamoja na nyaraka zake zote hivyo tuko tayari kuzingua kituo hicho asanteni sana na hongereni kwa kufungua fursa Mafinga,” amesema.

Kwa upande wake mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi amewapongeza wawekezaji hao kwa kuamua kuja kuwekeza katika mji wa kibiashara mafinga na kufungua fursa kwa watu wake.

Chumi alisema kuwa kufunguliwa kwa kitoa hicho licha ya kutoa ajira kwa watu wamafinga bali ni faida kwa Serekali itapata faida kwa kukusanya kodi.

“Miaka michache hapo nyuma mzee Mwinuka alitualika kule Njombe kwenye uzinduzi wa kituo kama hiKI,nikamwambia mzee mwinuka embu sogea na Mafinga tulete huduma hii, hatimaye leo lile nililomwambia limetimia niwashukuru sana,” Chumi.

Awali, akisoma risala ya uzinduzi huo, Daudi Mwinuka alisema kuwa lengo la kujenga kituo hicho ni kutoa huduma bora ya mafuta na vilainishi kwa ajili ya magari na mitambo kwa wakazi wa mji wa Mafinga na wasafiri na wasafirishaji wanaopita barabara kuu ya Iringa -Mbeya.

Hata hivyo, David ameshukuru serekali ya awamu wa sita chini ya uongozi thabiti wa, Rais Dk. Samia Suluh Hassan wa Tanzania kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wazawa kuweka shughuli za uwekezaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles