25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Corona yamliza Naomi Campbell kila siku

LONDON, UINGEREZA

STAA wa filamu na mitindo nchini Uingereza, Naomi Campbell, ameweka wazi kuwa kila siku amekuwa akilia kutokana na kupoteza marafiki kwa virusi vya Corona.

Virusi hivyo vya Corona vilianza kugundulika tangu Desemba mwaka jana huko nchini Korea Kusini, lakini sasa vimeenea sehemu kubwa ya dunia.

Naomi mwenye umri wa miaka 49, alitumia ukurasa wake wa Instagram na kudai kuwa, virusi hivyo vimekuwa vikiondoa idadi kubwa ya watu na miongoni mwa watu hao ni rafiki zake.

“Corona ni virusi hatari, dunia imesimama na kushangaa aina hii ya virusi ambayo inaondoa idadi kubwa ya watu, madaktari wanapambana lakini mambo bado, kikubwa ni kumuomba Mungu aweze kuondoa virusi hivyo, kila siku nimekuwa nikilia kwa kuwa napoteza marafiki zangu kutokana na virusi hivyo, kikubwa watu kufuata maagizo kutoka kwa wataalamu,” alisema mrembo huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles