28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Kahata ‘awamisi’ mashabiki Simba

WINFRIDA MTOI, DAR ES SALAAM

IKIWA bado hakuna dalili za kurejea kwa Ligi Kuu Tanzania, kiungo wa Simba, Francis Kahata, tayari ‘amemisi’ kelele za mashabiki wa kikosi hicho.

Kwa sasa Kahata yupo nyumbani kwao nchini Kenya baada ya ligi hiyo kusimama kutokana na agizo la serikali kuepuka kusamba virusi vya ugojwa wa Corona.

Tangu ametua nchini kwao, Kahata maeonekana akijihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwamo kutoa msaada wa maji na dawa za kunawia mikono ili kujikinga na Corona.

Pia nyota huyo anaonekana akijifua vikali katika maeneo ya nyumbani kwake kutokana na Kenya kuzuia watu kutoka kipindi hiki.

Katika ukurasa wake wa instagram jana, Kahata aliandika kuwa amezikumbuka kelele za mashabiki wa kikosi hicho hasa wanapokuwa uwanjani wakicheza mechi.

“Namisi sana kelele za mashabiki wa Simba, tukiwa uwanjani, kweli mna upendo wa ajabu, ” alisema Kahata.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles