22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

CIARA, TEKNO MILES WATOKA NA ‘Freak Me’

NEW YORK, MAREKANI


MKALI wa muziki na mitindo nchini Marekani, Ciara Harris, amethibitisha kuachia wimbo mpya ujulikanao kwa jina la ‘Freak Me’ aliyemshirikisha nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria, Tekno.

Mrembo huyo alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuweka wazi kuwa wimbo huo umeachiwa tangu Agosti 10 wiki iliyopita.

Posti hiyo ambayo aliiweka kwenye Instagram, ilimwonesha mrembo huyo akiwa na wasichana wengine wamevaa mavazi ya Kiafrika na kuandika: “Freak Me Ft Tekno, umeachiwa tangu Ijumaa, nimetumia nafasi hii kuwapa taarifa mashabiki zangu, muziki wa Kiafrika, mawimbi ya Kiafrika,” aliandika Ciara.

Mastaa wa nchini Nigeria wamekuwa wakipambana kuhakikisha wanaufanya muziki wao unavuka mipaka ya Afrika kwa kufanya kazi na wasanii wa Bara la Ulaya na sehemu nyingine, huku albamu mpya ya Drake ijulikanayo kwa jina la Scorpion ikisikika sauti ya Tekno.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles