26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Chokoraa: Redio zinazoiga zimeshusha muziki wa dansi

mapacha 16NA MWALI IBRAHIM

RAPA aliyerejea Bendi ya The African Star ‘Twanga Pepeta’ akitokea Bendi ya Mapacha Watatu, Khalid Chuma ‘Chokoraa’, amesema kuigana kwa redio za nchini kwa baadhi ya vipindi ndiko kunakochangia kwa kiasi kikubwa kuporomosha muziki wa dansi nchini.

Chokoraa anayetarajia kutangazwa rasmi Juni 4 kwa mashabiki wa bendi hiyo katika onyesho maalumu litakalofanyika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jana alitembelea ofisi za New Habari (2006) zinazochapisha gazeti hili pamoja na Bingwa, Dimba, Rai na The African.

Katika mazungumzo yake, alisema redio iliyokuwa ikipiga kwa kiasi kikubwa muziki wa dansi ilipoacha kupiga muziki huo na kugeukia muziki wa Bongo Fleva, redio nyingine nazo zikaiga redio hiyo jambo ambalo limesbabisha muziki wa dansi ukakosa nafasi ya kuchezwa redioni kama ilivyokuwa zamani.

“Awali walituambia kwamba nyimbo za dansi zinatumia muda mrefu wa zaidi ya dakika 10, tumepunguza kwa sasa nyimbo nyingi zinatumia chini ya dakika tano lakini bado hazipewi nafasi kama zamani hilo ni tatizo.

“Tunachoomba hali ile irudi redio zitenge vipindi vya kucheza nyimbo za dansi za nchini na pia waandishi wa magazeti nao waweke utaratibu wa kutumia angalau habari moja ya msanii wa dansi itasaidia kurudisha muziki huo kupendwa kama zamani,” alimaliza Chokoraa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles