30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

BMT yaonya wanaokwamisha uchaguzi Yanga

BMTNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limewaonya wanaohusika na vitendo vya kuhujumu uchaguzi wa klabu ya Yanga, vinavyofanywa ndani na nje ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) ili kukwamisha zoezi la uchukuaji fomu.

Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 25 mwaka huu lakini zoezi la uchukuaji wa fomu kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi umedorora.

Hadi sasa waliochukua fomu ni Aron Nyanda anayegombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti na Pascal Laizer na Edgar Chibura wanaowania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Mohamed Kiganja, alisema baraza hilo limesogeza mbele muda wa kuchukua fomu hadi Juni 5 mwaka huu badala ya jana jioni kama ilivyopangwa.

“Kuna mtu mmoja (hakumtaja jina) ametumwa kuvuruga zoezi la uchukuaji fomu, hivyo ni vyema akaacha mara moja ili uchaguzi wa Yanga ufanyike kwa mafanikio kama ilivyotarajiwa, kwa bahati mbaya wanaohangaika ili kukwamisha mchakato huu wanatoka ndani na nje ya TFF.

“Tuliagiza fomu zitolewe mapema kwa njia ya mtandao ili kila anayetaka kugombea achukue na kulipia benki, lakini mambo yamekuwa tofauti na maelekezo kwa makusudi,” alisema Kiganja.

Kiganja aliongeza kuwa licha ya hujuma zinazofanywa uchaguzi lazima ufanyike kama ulivyopangwa ili klabu ya Yanga iweze kupata viongozi halali watakaoongoza kwa miaka minne ijayo.

“Mambo yanayoratibiwa kuelekea uchaguzi si utashi wa mtu bali ni kutekeleza katiba ya Yanga kwa kufuata demokrasia, hivyo vikao vya wanachama au wadau vinavyofanyika vinatakiwa kulenga mafanikio ya uchaguzi badala ya kuvuruga,” alisema Kiganja.

Katibu huyo alisisiza kuwa kadi za zamani za wanachama ndizo zitatumika kwenye uchaguzi huo.

“Mwanachama ambaye hana kadi ya zamani na anataka kupiga kura inabidi akalipie mwaka mmoja ili aruhusiwe, kwani kadi ya benki haiwezi kutumika kwa kuwa haitambuliki,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles