29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

CHINA YAKATAA KUIPIGIA MAGOTI MAREKANI

BEIJING, CHINA                  |           


WIZARA ya Biashara ya China imetangaza msimamo wa Serikali ya nchi hiyo dhidi ya Marekani, ambapo imemuonya Rais Donald Trump na kusisitiza kuwa haitaipigia magoti katika vita yao ya kibiashara inavyoendelea sasa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa jana mjini Beijing na wizara hiyo imemkosoa Rais Donald Trump ambaye ameamua kuongeza ushuru wa forodha wa dola bilioni 16 kwa bidhaa kutoka China zinazoingizwa nchini Marekani, hali ambayo inadaiwa kuchochea uhasama na uhusiano mbovu wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo. Awali Serikali ya Marekani iliipandishia China ushuru wa forodha wa dola bilioni 34.

Katika taarifa hiyo, China inamtuhumu moja kwa moja Trump kuwa serikali yake inakusudia kuvuruga muundo wa kiuchumi uliopo na kukiuka sheria za Shirika la Biashara Duniani na hivyo kusababisha kuibuka makundi, mpasuko wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za dunia.

Msemaji wa Wizara ya Biashara ya China, Gao Feng, amekosoa mwenendo wa Shirika la Biashara Duniani katika vita vya kibiashara vya Marekani na kusema kuwa hali ya sasa inalazimu kufanyiwa marekebisho shirika hilo na kwamba Rais Xi Jingping anaunga mkono marekebisho hayo.

Vita ya kibiashara kati ya Marekani na China vilianza Machi 8 mwaka huu, kufuatia uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuzidisha ushuru wa forodha kwa bidhaa za China zinazoingizwa nchini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,335FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles