24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

WAFUASI 75 WANYONGWA MISRI

CAIRO, MISRI                     |           


MAHAKAMA Kuu nchini Misri jana imetoa hukumu ya kunyongwa wafuasi 75 wa Chama cha Muslim Brotherhood na sasa hukumu hiyo inasubiri idhini ya Mufti wa nchi hiyo kabla ya kutekelezwa.

Taarifa inasema, mahakama hiyo ambayo ilikuwa na kikao chake mjini Cairo chini ya uwenyekiti wa Jaji Hassan Farid, imetoa hukumu baada ya kusikiliza kesi ya wafuasi wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Mohammad Mursi,

Washtakiwa hao wamehukumiwa kunyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kuandamana bila kibali mwaka 2013  katika Kitongoji cha Rabaa Adawiya, mjini Cairo.

Maandamano hayo yalifanyika baada ya jeshi, chini ya uongozi wa Rais wa sasa wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi, kumtimua  Mursi kupitia njia ya mapinduzi. Katika makabiliano yaliyojiri katika maandamano hayo yaliyokusudia kulalamikia kitendo cha kupinduliwa Rais Mursi, mamia ya watu waliuawa wakati jeshi likitawanya waandamanaji.

Kati ya waliohukumiwa kifo na mahakama hiyo ni viongozi waandamizi wa Mohammad Al Beltagui, Essam Al Erian, Abdul Rahman Al Bar na Osama Yassin.

Baada ya Mursi kupinduliwa, chama chake cha Muslim Brotherhood kilitangazwa kuwa kundi la kigaidi na wafuasi wake wengi, akiwemo Mursi mwenyewe wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka katika mahakama za nchi hiyo huku wengi wakihukumiwa kunyongwa.

Baada ya kupinduliwa Mursi, Rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Misri, nafasi yake ilichukuliwa na El Sisi ambaye anawakandamiza wapinzani kwa kutumia mkono wa chuma, jambo ambalo limepelekea ghasia na machafuko kuenea katika nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles