23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

China yaipiga tafu Tanzania vifaa vya mafunzo ya Uvuvi

Na Christina Galuhanga, Mtanzania Digital

Serikali ya Tanzania hii imepokea msaada wa vifaa vya mafunzo ya uvuvi na uchakataji wa samaki kwa ajili ya Chuo cha Ufundi stadi cha wilaya ya Chato wenye thamani ya Sh milioni 350 uliotolewa na serikali ya watu wa China.

Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Wang Ke pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako wakishuhudia na watendaji wengine wakati wakisauhi makabidhiano ya vifaa vya mafunzo ya uvuvi na uchakataji samaki kwa ajili ya Chuo cha Ufundi Stadi Veta Wilaya ya Chato vilivyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.

Akizungumza Mei 25, 2021 wakati wa hafla hiyo jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amesema msaada huo ni muhimu sana kwa chuo cha Halmashauri hiyo kutokana na chuo hicho kuwa cha kwanza nchini kwa kutoa mafunzo ya uvuvi na uchakataji samaki.

Aidha amewataka wakufunzi wa chuo hicho kuhakikisha wanavitunza vema vifaa hivyo ili vitumike kikamilifu na kusaidia wanafunzi ambao watakuwa wataalamu mahiri katika nyanya ya uvuvi na uchakataji wa vifaa vya uvuvi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Veta, Pankras Bujulo amesema vifaa hivyo ni matokeo ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa china mara baada ya kuja nchini na kufika katika chuo na kuahidi kukisaidia ili kikue kitaaluma.

Naye Balozi wa China nchini, Wang Ke amesema msaada huo wa vifaa ni mwendelezo wa ushirikiano wa china na Tanzania,kila taifa linategemea elimu ili kuzalisha watu watu wenye weledi wa kutosha katika fani mbalimbali na kusaidia taifa kukua kiuchumi.

Ameongeza kuwa serikali ya China inajionea fahari kuendelea kuisaidia Tanzaniana ili kuhakikisha watu wake wanaendelea na kupata kizazi kilichoendelea chenye manufaa makubwa.

Leonard Akwilapo ni Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo amesema ukizingatia uhaba wa vifaa uliokuwepo, vifaa hivyo vitasaidia pakubwa kuendeleza chuo na wanafunzi kuweza kupata elimu yenye viwango vyakutosha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles