23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Chanzo kifo cha Gamba chasubiri uchunguzi wa daktari

Mwandishi wa Wetu



Sababu ya kifo cha aliyekuwa mtangazaji wa Deustche Welle (DW), Isaac Gamba, aliyefariki ghafla nyumbani kwake nchini Ujerumani, inasubiri ripoti ya daktari.

Akizungumza na Mtanzania Digital kutoka Bon nchini Ujerumani, mtangazaji mwenziwe Gamba, Sudi Mnette, amesema hadi wakati huu chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika na wanasubiri ripoti ya daktari baada ya uchunguzi.

Sudi amesema Gamba amefariki ghafla na hadi sasa haijafahamika chanzo cha kifo chake kwani hadi Jumatatu alikuwa kazini akiwa sawa sawa wala hakuonyesha dalili yoyote kama alikuwa na ugonjwa wowote.

“Alikuwa sawa tu, wala hakuwa na dalili kama alikuwa mgonjwa, alikuwa ametoka kazini Jumatatu asubuhi na tukabishana sana kuhusu siasa, kuna waliobahatika kuzungumza naye kwenye simu.

“Hadi jana hatukupata mawasiliano naye, leo ndiyo imedhihirika baada ya kwenda nyumbani kwake na kukuta amefariki, si unajua huku kila mtu na kazi na mambo yake.

“Mimi ni kaka yangu amenikuta kazini nikamtembeza kwenye ngazi za Ulaya, na mimi nilimkuta Radio Uhuru,” amesema Mnette.

Kwa habari zaidi endelea kusoma Mtanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles