25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Milioni 500 zatumika kuboresha miradi ya maji Temeke

                    Tunu Nassor,Dar Es Salaam



Naibu Waziri wa Maji,Jumaa Aweso ameagiza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA), kuelekeza nguvu kupeleka maji katika maeneo ya pembezoni mwa jiji hilo ili kuwafikia wananchi wa hali ya chini.

Aweso ameyasema hayo leo Alhamisi Oktoa 18, katika uzinduzi wa miradi ya maji safi Kibondemaji na wa kuchakata maji taka uliopo Toangoma Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam na ameiomba Dawasa kuongeza nguvu katika maeneo ya pembeni mwa jiji kwa kuwa hayana maji.

“Maeneo mengi ya Temeke, Ukonga, Segerea na Kigamboni hayana maji hivyo ongezeni jitihada za kuhakikisha yanapata maji safi na salama,” amesema Aweso.

Aweso amesema mradi huo wenye jumla ya urefu wa Kilometa 11 na kisima chenye urefu wa Mita 180 umegharimu Sh Milioni 546 na itawanufaisha wakazi wa Temeke, umetekelezwa  na Water Aid ukisimamiwa na Shirika la Maendeleo ya Watu (PDF) na kukabidhiwa kwa Dawasa.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema Mamlaka hiyo inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika maeneo ya pembezoni ili kuhakikisha wanapata maji ya uhakika.

“Tumeweza kuondoa tatizo la Kipindupindu kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa miaka mitatu sasa kutokana na upatikanaji wa Majisafi na salama,” amesema Luhemeja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles