26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

CHANJO YA MALARIA KUANZA AFRIKA

GENEVA, USWISI


CHANJO ya kwanza duniani dhidi ya ugonjwa wa malaria itaanza kutolewa kwa nchi tatu za Ghana, Kenya na Malawi kuanzia mwaka 2018.

Chanjo hiyo ya RTS huipa nguvu kinga ya mwili ili iweze kushambulia viini vya malaria ambavyo husambazwa na mbu.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kuwa chanjo hiyo ina uwezo wa kuokoa maisha ya maelfu ya watu.

Lakini bado haijabainika iwapo inaweza kutumika kati nchi masikini zaidi duniani.

Mtu anastahili kupewa chanjo hiyo mara nne, huku tatu za kwanza zikitolewa kila mwezi kipindi cha miezi mitatu kabla ya kumalizia chanjo ya nne miezi 18 baadaye.

Mafanikio haya yamepatikana kufuatia majaribio yaliyopata ufadhili mkubwa, lakini haijulikani bado iwapo yanaweza kufanyika katika nchi ambazo huduma za afya ni duni.

Ni sababu hiyo iliyoifanya WHO ianze majaribio hayo katika nchi tatu kubaini iwapo mpango mzima wa utoaji chanjo hiyo unaweza kuanza.

Mpango wa utoaji chanjo hiyo utawahusisha zaidi ya watoto 750,000 walio na umri wa kati ya miezi 5 na 17.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles