26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Chama cha Waoka mikate chalia na Serikali

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Mwenyekiti wa Chama Cha Waokaji wa Mikate na keki Tanzania(TBA), Francisca Lyimo ameiomba Serikali kupunguza gharama za bidhaa wanazotumia kuzalisha mikate.

Akizungumza wakati wa kufunga maonyesho ya kuoka mikate Tanzania yaliyofanyika Katika maonyesho ya 46 ya Biashara maarufu kama Sabasaba,Francisca amesema kupanda kwa kodi,unga na mafuta imekuwa ni changamoto kubwa kwa wafanyabiashara hao.

“Chama chetu kinakabiliwa na changamoto kubwa ya upandaji wa gharama za vifaa kama unga na mafuta hali inayosababisha kupungua kwa soko la uzalishaji,” amesema Lyimo.

Amesema chama hicho kinaungana na Sido katika kutoa mafunzo ya namna ya uandaaji na kupika mikate hiyo kwenye kiwango kinachotakiwa.

Amefafanua zaidi kuwa katika maonyesho hayo zaidi ya 15 walishiriki mashindano hayo na bidhaa 80 zilipikwa kwa ajili ya kuonyeshesha kuonjesha Watanzania.

Aidha, mbali na maonyesho hayo chama kinatoa elimu kuhusu ubora wa bidhaa na kujiepusha kutumia bidhaa zisizo na ubora.

Akizungumza katika maonyesho hayo mke wa Waziri Mkuu msaatafu wa Tanzania, Tunu Pinda amewataka TBA kuendelea kutangaza bidhaa zinazozalishwa na Watanzania kwa maslahi ya nchi.

Aidha, amewataka wanachama hao kuandaa siku maalum ya mafunzo uokaji.
Amesema ni vyema kuendelea kutumia majukwaa ya biashara ili kujiendeleza kidigital.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles