26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi ya Roijo yazindua Siku ya Batiki Tanzania

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Roijo Progress Center ikishirikiana na Serikali imezindua siku ya Batiki Tanzania ambayo inalenga kufungua fursa za uuzaji wa batiki ndani na nje ya nchi.

Uzinduzi wa siku hiyo ya batiki umefanyika juzi katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Rose Urio, amesema lengo lake ni kuitangaza batiki katika soko ndani na nje ya nchi pamoja na kumpatia mwanamke kuitumia fursa hiyo kujiingizia kipato.

“Tunafahamu kwamba batiki ni fursa ya kibiashara ambayo inafanywa na mtu yeyote, lakini hapa tunataka mwakamke ndiye aichangamkie zaidi ili imsiadie kujikwamua kiuchumi,” amesema Rose.

“Miasha yamebadilika, thamani ya mwanamke ni kujitegemea kiuchumi, batiki ni bidhaa ambayo inaweza kuzalishwa hata katika eneo dogo lenye uwazi, kwa hiyo tunawahamasisha wanawake waingie kwenye fursa hii,” amesema Rose.

Amefafanua kuwa katika mradi huo wa batiki, wanatarajia kuzinda ua maalum linalojulikana kama‘Ua la Mama’ ambalo lengo lake litakuwa ni kumuenzi Rais Samia Suluhu Hassan.

“Tumejipanga kuhakikisha kwamba tunaboresha zaidi batiki zetu, mpaka sasa hatuna Standard za batiki zinazofanana, tunazozizalisha sasa ni zile ambazo unakuta mmoja na mita mbili na nusu, mwingine tatu au nne kabisa, kwa hiyo tunataka tupate standard moja,” amesema Rose.

Ameongeza kuwa kupatikana kwa viwango vya bidhaa hiyo, itasaidia kuviuza na kushindana katika soko la ndani na nje ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles