29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 28, 2024

Contact us: [email protected]

Chadema yatumia mabango kufikisha ujumbe Mwanza

Na Mwandishi wetu, Mwanza

Jiji la Mwanza leo Februari 15, 2024 limeendelea kuwa katika hali ya utulivu licha ya kufanyika kwa maandamanc Chama Cha Demokrasia  na Maendeleo (Chadema) yenye lengo la kuishinikiza Serikali kutatua changamoto zinazowatesa wananchi ikiwemo  gharama za maisha kuwa juu pamoja na kudai Tume huru ya Uchaguzi.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, Mwabukusi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Azavel Lwaitama, John Heche, Benson Kigaila na Twaha Mwaipaya ni miongoni mwa viongozi walioongoza maandamano hayo yaliyoanzia Buhongwa saa 4.40 asubuhi kuelekea uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza ambao wamezungumza na Mtanzania Digital kuhusu maandamano hayo wamekuwa na mitazamo tofauti huku baadhi wakisifu mbinu iliyotumiwa na Chama hicho Kikuu cha Upinzania nchini ya kutumia mabango kufikisha ujumbe kwa Serikali.

“Tumevutiwa na mbinu hii iliyotumiwa na Chadema katika maandamanio ya hapa Mwanza kwani inapunguza vurugu badala yake ujumbe unafika ulikokusudiwa huku wananchi wakiendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa,” amesema John Lushona mkazi wa Buhongwa jijini humo.

Henry Faustine Mkazi wa Ilemela na Pendo Joseph Mkazi wa Wilayani Nyamagana wamesema kuwepo kwa maandamano hayo kutasaidia kuishinikiza Serikali kupunguza ugumu wa maisha kwa kushusha bei za bidhaa mbalimbali ikiwemo sukari ambayo kwa sasa inauzwa Sh 4,000 hadi 4,500 kwa kilo moja.

“Nawapongeza sana Chadema kwa kuratibu maandamano haya naamini hadi wamalize mikoa yote Serikali itakuwa imesikia na kutatua baadhi ya changamoto ambazo wananchi tunalalamikia, maisha ni magumu kwa kweli lakini sukari jamani sukari ni tatizo bei iko juu sana, sabuni nayo ni shida, sisi wenye kipato cha chini tunateseka sana,” amesema  Pendo.

Wafuasi wa Chadema na viongozi mbalimbali wa chama hicho wameshiriki kwenye maandamano ya amani  yaliyohitimishiwa uwanja wa Furahisha wakiwa wametanguliwa na baadhi ya bodaboda huku wakiwa wamenyanyua bendera za Chama Chao juu wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema  Taifa Freeman Mbowe wakishinikiza serikali kupunguza gharama za maisha, Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles