23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

CCM yajipanga Dodoma, ACT Wazalendo Z’bar

 WAANDISHI WETU– DODOMA/ZANZIBAR

HEKAHEKA za Uchaguzi Mkuu zinaelendelea kupamba moto, huku vyama vya siasa vikindelea kujipanga kutafuta wadhamini wa kuwaunga mkono, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepiga kambi jijini Dodoma kukamilisha michakato yake ya ndani ya kupata wagombea ubunge wa majimbo na viti maalumu nacho Chama cha ACT Wazalendo kimepiga kambi Visiwani Zanzibar.

ACT Wazalendo, imepiga kambi visiwani humo baada ya jana wagombe wake wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bernard Membe na mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kupokewa na mamia ya wafuasi wao.

Hata hivyo,CCM kimekuwa kwenye mchakato kwa jumuiya zake kufanya uchaguzi wa kupata wabunge wa makundi ya vijana, wazazi na wanawake ambao majina yao yatapelekwa mbele ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kwa uamuzi wa mwisho kabla ya kuwasilishwa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Juzi Jumuiya ya vijana ilikamilisha mchakato wake wa kupata wabunge wao 10 ambapo kwa upande wa Bara ni Lulu Mwacha, Halima Bulembo, Juliana Masaburi, Lucy Sabu, Asia Hamlaga na Judith Kapinga.

Huku kwa wabunge vijana kutoka Zanzibar waliochaguliwa ni Munira Mustafa Khatib, Latifa Khamis Juakali, Amina Bakari Yusuf na Amina Ali Mzee.

Kwa siku ya jana,Jumuiya ya Wazazi ilikuwa ikifanya uchaguzi wa kupata wawakilishi wao wa viti maalumu kupitia jumuiya hiyo.

Uchaguzi huo, ulikumbwa kwa sintofahamu baada ya karatasi za kura kukosewa picha na majina ya wagombea jambo lililofanya kusimama kwa muda ili kuruhusu marekebisho na ilipofika saa 8 mchana uliendelea kwa wajumbe kupiga kura ambapo leo ni zamu ya Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) ambao nao wataendelea na mchakato wao.

Jiji la Dodoma kwa sasa limefurika wagombea mbalimbali wa ubunge wa majina pamoja na viti maalumu huku wengi wao wakipita huku na kule kushawishi wajumbe wa Kamati Kuu na NEC ili majina yao yaweze kurudishwa kwenda kugombea nafasi za ubunge majimboni.

 ACT YAIFUNIKA ZANZIBAR

Jana mamia ya wanachama wa ACT Waazalendo Kisiwa cha Unguja, wamejitokeza kuwapokea wagombea wa chama hicho wakitokea Tanzania Bara kwa kupitia bandari ya Zanzibar .

Mapokezi yalianza Bandari ya Malindi kupitia njia ya Darajani, Kisiwandui, Michenzani na kupitia njia ya Madema, Maisara na kumalizikia katika ofisi kuu ya chama hicho iliyopo Vuga,

Wanachama hao wakiwa katika eneo la Mkunazini walizuiwa na jeshi la polisi ili wasipandishe juu kuelekea Michenzani na badaye jeshi hilo lililazimika kuondoa kizuizi hicho.

Akizungumza na wanachama na wafusi wa chama hicho jana, mgombea urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad alilitaka jeshi hilo kuacha upendeleo katika kusimamia sheria kupitia vyama vya siasa.

“Vyama vyote vya siasa ni sawa hakuna chama ambacho kiko juu ya sharia kwa maana hiyo jeshi la polisi linatakiwa kutenda usawa kwa vyama vyote,” alisema.

Alisema imekuwa ni kawaida chama cha upinzani kinapofanya shughuli zake kupata vipingamizi vikubwa kutoka kwa jeshi hilo jambo ambalo alidai ni kinyume na sheria. Alitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC ), kuacha ushabiki wa kisiasa katika kutekeleza majukumu yao ili kuepusha kuutia dosari uchaguzi unaokuja.

Kwa upande wa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania kupitia chama hicho, Bernard Membe aliwataka wanachama wa chama hicho kujipanga ili kuhakikishsa wanashinda vita vilioko mbele yao.

Alisema endapao watapata ridha ya wananchi ya kuongoza dola atahakikisha Zanzibar inakuwa na mamlaka yake ya kuamua mambo yake yote.

“Haiwezekani leo masheikh wakamatwe Zanzibar, halafu wahamishiwe Tanzania bara ni sawa na kuzitusi mahkama za Zanzibar katika Serikali yetu ni lazima Mahakama za Zanzibar ziwe na hadhi yake kama zilivyo mahakama za bara,” alisema 

Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe alisema amani ya Zanzibar ipo kwenye mikono ya Tume ya Uchaguzi, kwani chombo hicho kikikosea kimevuruga amani iliyopo.

“Lazima waendeshe uchaguzi ambao ni huru na wa haki ili kuepusha uvunjifu wa amani usitokee ya katika nchi zetu,” alisema. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles