25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

JPM afanya uteuzi mwingine

 MWANDISHI WETU– DODOMA

RAIS Dk. John Magufuli, amefanya uteuzi wa lala salama ikiwa zimebaki siku chache kuanza kwa kampeni cha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Taarifa iliyolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, ilieleza kuwa Rais Magufulim amemteua Ng’wilabuzu Ludigija kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam.

Kabla ya uteuzi huo, Ludigija alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Mussa Chogelo ambaye amepangiwa kazi maalumu katika Ofisi ya Rais.

Kufuatia uteuzi huo, Rais Magufuli amemuhamisha kituo cha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi, Erasto Kiwale ambaye anakwenda kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam.

Kiwale anachukua nafasi ya Ng’wilabuzu Ludigija ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala.

 Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Catherine Mashalla kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi.

Kabla ya uteuzi huo, Mashalla alikuwa Ofisa Elimu wa Manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam na anachukua nafasi ya Erasto Kiwale ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni.

Uteuzi na uhamisho wa viongozi hao umeanza jana Agosti 9, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles