22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

CCM Tabora yatangaza ushindi wa asilimia 95

Allan Vicent -Tabora

ASILIMIA 95 ya wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoani Tabora, wamepita bila kupingwabaada ya vyama vya upinzani kususia uchaguzi huo.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, Solomon Kasaba, alipokuwa akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana.

Alisema hata kabla ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi huo wa viongozi wa mitaa, vitongoji na vijiji, tayari asilimia 95 ya wagombea wa CCM wamepita bila kupingwa na asilimia tano ndo watafanya uchaguzi.

Alisema kati ya vijiji 715 vya mkoa huo, CCM imepita bila kupingwa kwenye vijiji 675 ikiwa ni ushindi kwa asilimia 94.7 na uchaguzi utafanyika katika vijiji 38 tu sawa na asilimia 5.3.

Alisema kakati mitaa 148 ya mkoa huo, wagombea 140 wa CCM wamepita bila kupingwa ikiwa ni ushindi wa asilimia 94.5 hivyo uchaguzi utafanyika kwenye mitaa nane tu ambayo ni sawa na asilimia 5.5.  

Solomoni alisema kati ya vitongoji 3,619 vya mkoa mzima wamepita bila kupingwa kwenye vitongoji 3,397 sawa na asilimia 94 hivyo uchaguzi utafanyika katika vitongoji 228 tu sawa na asilimia 6.

 “Hadi sasa tumeshashinda kwa zaidi ya asilimia 95 na tuna uhakika hata hizo asilimia 5 zilizobakia tutazichukua zote kwa kuwa wagombea wa upinzani waliopo hawazidi 10 na hawana sera yoyote na hata kampeni hawafanyi,” alisema.

Solomon alitaja vyama vitakavyochuana na CCM kuwania nafasi hizo kwa baadhi ya maeneo kuwa ni NRA, CCK, Chadema, CUF, Democratic Party, Demokrasia Makini, NCCR-Mageuzi na ADA TADEA, huku akibainisha kuwa baadhi vilizindua kampeni tu vikaishia mitini.

Alisisitiza kila chama kina haki sawa ya kidemokrasia ya kuomba kuchaguliwa na wananchi kupitia mikutano ya kampeni na kuongeza kuwa wataendelea kufanya kampeni zao kistarabu ili wazoe viti vyote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles