22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

CCM Njombe yawataka wananchi kuchukua tahadhari ya corona

Na Mwandishi Wetu, Njombe

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Njombe kimetaka wananchi mkoani humo kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa COVID 19 kwa kuzingatia uvaaji barakoa,vitakasa mikono na kuepuka mikusanyiko.

Akizungumza na wandishi wa habari Katibu wa Siasa na Uenezi mkoa wa Njombe, Erasto Ngole, alisema corona ipo nchini kama Rais Samia Suluhu alivyosema, hivyo kila mwananchi achukue tahadhari.

“Rais ametuelekeza juu ya ugonjwa wa corona, lazima niwaambie ndugu zangu hata Njombe corona ipo na serikali imekuwa wazi tuchukueni tahadhari,”alisema Ngole.

Ngole pia alizungumzia swala la katiba pya alisema hivi sasa siyo kipaumbele cha serikali ya awali ya sita ambapo juhudi zinazofanyika ni kutatua changamoto zinazowakabili watanzania kwa kusimamia miradi ili Ilani itekelezwa kikamilifu.

“Katiba mpya sio kipaumbele cha watanzania kwa sasa wala sio kipaumbele cha serikali ya awamu hii, kipaumbele ni kutatua changamoto zinazowakabili wananchi, tumejikita kutekeleza ilani ya CCM ambayo ndio deni letu kwa wananchi, katiba mpya itakuja baada ya kupunguza mzigo wa changamoto unaowakabili watanzania,” alisema Ngole.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Isaya Mwasubila alisema serikali kupitia watalaamu wa afya wanaendelea kutoa elimu ya kujikinga na corona huku akiagiza maeneo ya ofisini na kwenye mikusanyiko kuhakikisha wanaweka ndoo za maji ya kunawa,kuvaa barakoa.

“Ni tahadhari ambazo zinaendelea kuchukuliwa ikiwemo na zile za awamu ya kwanza, pia kwenye awamu hii ya tatu hatua ni zile zile ikiwemo kunawa mikono kwa maji safi na tiririka pia kuepuka misongamano,” alisema Mwasubila.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles