30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tigo yatoa fedha za matibabu miguu pinde

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya Tigo imetoa kiasi cha Sh milioni 220 kwa Hospitali ya CCBRT, kama sehemu ya kujitolea kwake kusaidia kituo cha afya katika kutokomeza tatizo la miguu pinde kwa Watanzania.

Mchango huo pia hutumika kama mpango wa uhamasishaji kwa umma juu ya umuhimu wa kufuata matibabu ili kuhakikisha wenye matatizo wanapona na kuzuia ulemavu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Julai 12, 2021, Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari amesema: “Mchango wetu unathibitisha zaidi kujitolea kwetu kusaidia jamii zinazotuzunguka.

“Matibabu ya miguu pinde nchini ni mada ambayo inahitaji utangazaji na kama kampuni ya simu inayoheshimika, tuko hapa leo kubadili hadithi, tunahitaji ushiriki wa jamii na nguvu ya kuhakikisha kwamba kila mtoto aliye na miguu pinde Tanzania, anapata matibabu bora na kwa wakati kwa kutumia njia ya Ponseti, kama matibabu ya kiwango cha juu na hivyo kuwapa fursa sawa ya kuishi maisha yenye tija kama walivyo wengine,” amesema Karikari.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi, aliishukuru Tigo kutokana na msaada huo endelevu ambao umekuwa ukisaidia kuokoa maisha ya watoto wengi Watanzania.

“Tigo Tanzania imeonyesha mfano kwa jukumu muhimu ambalo sekta binafsi imeamua kulichukua katika kuhakikisha inapunguza na kutatua shida za jamii.

“CCBRT, kwa miaka mingi imeweza kushughulikia moja ya mambo magumu zaidi ya matibabu ya miguu pinde, kuhakikisha matibabu yanakuwa endelevu na ufuatiliaji, kupitia uvumbuzi na msaada wa Tigo, kuna jukwaa la kukumbushana kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS), la CCBRT linaweza kutuma njia ya simu za mkononi kukuza ufuatiliaji ili wagonjwa watibiwe kikamilifu, bila athari yoyote.

“Kwa hivyo ningependa kuwahimiza sekta binafsi kuendelea kutupatia misaada ili kuhakikisha tunatokomeza tatizo hili na kulimaliza kabisa,” alisema.

Miaka mitatu iliyopita ya ushirikiano huu imeshuhudia karibu kesi 1,500 mpya za miguu pinde kwa watoto, wanaofaidika na matibabu ya miguu yanayobadilisha maisha kwa njia ya Ponset na mamia wamefanyiwa upasuaji CCBRT.

Katika miaka ya hivi karibuni, kesi hizo zimezidi kupungua na kwamba CCBRT inaendelea kufuatilia kwa ukaribu kwa ajili ya kuhakikisha wanafikia malengo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles