22.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Ukosefu wa maji yatajwa chanzo cha uvunjifu wa ndoa Njombe

Na Mwandishi Wetu, Njombe

Wananchi wa kata ya Masasi iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe wamelalamikia kuwa kukosekana kwa maji ni chanzo kikubwa cha migogoro ya ndoa na wakati mwingine imesababisha kuvunjika kwake.

Hayo yalisemwa na wananchi hao jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika vijiji vya Lihagule, Kiyoga na Kingole mbele ya mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga.

Walisema kwa muda mrefu upatikanaji wa maji safi na salama kwenye kata hiyo ni mdogo kiasi kwamba kila siku wanalazimika kuamka saa kumi na moja asubuhi kufuata maji na kurudi saa saba mchana hali inayopelekea migogoro katika ndoa.

Walisema kutokana na kutumia muda mrefu kwenye kutafuta maji wanawake wengi wamekuwa hawahaminiki kwa wanaume zao na wamekuwa wakituhumiwa kuwa wanatumia muda huo katika kufanya vitendo vya u malaya.

Walisema hata hivyo kazi nyingine zinashindwa kufanyika kwa wakati katika kata hiyo kutokana na muda mwingi kutumia katika kutafuta maji.

Waliiomba serikali kuimarisha miundo mbinu ya maji katika kata hiyo ili waweze kupata maji na kuondokana na changamoto hiyo inayowatesa na kuleta migogoro.

Baadhi ya wananchi wa kata hiyo akiwemo Selina Maundi na Catherine Haule walisema bomba wwaliloliweka kupeleka maji kutoka bomba kuu kwenda kwenye tenki ni dogo hivyo lina shindwa kusukuma maji.

“Tunaomba waturejeshee bomba la mwanzo kwani lilopo ni dogo na linashindwa kusukuma maji kwenda kwenye tenki ” alisema Selina.

Mhandisi wa maji kutoka wilayani Ludewa Mlenge Nasibu alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya maji katika kata hiyo na kusema kwa sasa wapo kwenye ukarabati wa mabomba kutoka njia kuu na utakapo kamilika wataanza kupata maji.

“Nilikweli tulileta bomba kutoka bomba kubwa kwenda kwenye tenki sasa tuna mpango wa kulibadilisha na kulileta kubwa,” alisema Nasibu.

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga alisema mwaka huu alikwenda kuomba fedha kwa ajili ya maji na serikali imetoa kwanza katika kijiji cha Kiyogo.

Alisema ataendelea kuiomba serikali ili iweze kutenga bajeti ya maji Kwa ajili ya vijiji vingine vyenye changamoto hiyo ya maji na kuhakikisha inapungua.

“Nitakwenda kumuomba waziri au naibu waziri wa maji waweze kutembelea kata ya Masasi ili kujionea hali halisi ya kero ya maji, na ningependa kuona serikali inatumia ziwa Nyasa katika kuleta maji kwenye vijiji kama ambavyo ilifanyika katika ziwa Victoria,” alisema Kamonga.

Alisema kuwa anaamini serikali iliyopo madarakani ni sikivu hivyo itakwenda kufanyia kazi ushauri huo na kuahidi kuendelea kuikumbusha serikali ili iweze kutekeleza mapema jambo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles