23.3 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

CALISAH: SITASAHAU ‘NILIPOENDESHA’ GHAFLA NYUMBANI KWA WEMA

NA CHRISTOPHER MSEKENABIASHARA ya mitindo (modeling) imeendelea kukua kwa kasi kubwa ulimwenguni kote huku Bongo ikiwakilishwa na wanamitindo wa kike wengi zaidi kuliko wa kiume.

Uchache wa wanamume kwenye tasnia hiyo imekuwa fursa kwa kijana Calisah Abdulhameed, modo mwenye ndoto nyingi za kuipeleka mbali sanaa ya mitindo kutoka Tanzania.

Calisah ambaye ni bosi wa kampuni ya uwakala wa warembo kwenye video za muziki (video vixen), magari ya kifahari na maeneo (location) nzuri za kufanyia video inayoitwa 0+ Door Company Limited amekutana na Juma3tata na kupiga stori kadhaa ili wewe ambaye umeanza kumfahamu baada ya kutoka kimapenzi na Wema Sepetu upate kutambua usiyoyajua kuhusu modo huyu, karibu…

Juma3tata: Calisah ni nani?

Calisah: Mimi ni mtoto wa mwisho kwenye familia ya watoto watano wa Mzee Abdulhameed, nina kaka zangu wawili ambao ni Hassan na Osman na dada zangu  Ashuu na Lucsein.

Juma3tata: Safari yako kwenye mitindo ilianzia wapi na lini?

Calisah: Rasmi niliingia kwenye 'Modeling' mwaka 2012, nilimsindikiza rafiki yangu kutumbuiza kwenye shoo ya Clouds inaitwa After School Bush. Kutatokea kipengele cha Mr & Miss XXL, mimi nilikuwa 'Backstage' watu walinishawishi nishiriki kwenye kipengele hicho, nikapanda jukwaani na nikashinda,  mwaka wa nyuma alishinda Hamisa Mobetto na mwaka huo nikashinda mimi.

Juma3tata: Uliitumiaje fursa ya kuwa Mr xxl?

Calisah: Nilikutana na Martin Kadinda, sikudhani kama atanifahamu, akaniambia nina mwanekano mzuri kwanini nisiwe modo, nikamwambia natamani kufanya ila sijui pa kuanzia, alinishika mkono akanipeleka kwa mwanamitindo Asya Idarous, mama alinipokea akawa ananichukua kama mwanaye, nikafanya shoo yake ya kwanza Lady In Red baada ya hapo nikashiriki maonyesho ya Maridadi, Kanga za Kale, Swahili Fashion nk, nikafikiria kufanya video za muziki ili nizidi kuji-brand, nikafanikiwa kufanya video kama 15 ambazo zingine nilifanya bure, zingine nilikuwa napewa tu nauli.

Juma3tata: Ulipata chochote baada ya kuwekeza muda wako kwenye mitindo na video za muziki?

Calisah: Nipata dili za kufanya matangazo kadhaa kwenye kampuni za mitandao ya simu pia nikaja kuwa balozi wa Oxfam hapa nchini.

Juma3tata: Maisha yako kabla hujaingia kwenye mitindo yalikuwa vipi?

Calisah: Nimepitia mambo mengi magumu, unajua sina wazazi mama yangu alifariki nikiwa na miaka 6, baba pia akafa mwaka 2009, nikalelewa muda mrefu na bibi na nikaja kupata shida nilipoishi na mama yangu wa kambo, nili-experience maisha ya tabu ya kupigwa, kutumwa, kulala njaa, kutaka kuwekewa sumu kwenye chakula nk.

Juma3tata: Huwezi kusahau nini kwenye maisha hayo?

Calisah: Siwezi kusahau mama wa kambo aliniponifukuza nyumbani, nikaanza kulala kwa washkaji, nilishauza nguo za mitumba Kariakoo, nimelala nje ya maduka ya watu wengi wenye maduka makubwa ya nguo kama kina Chid Mapenzi,  Roby One na wengine nilishakutana nao sana chimbo kugombania nguo za kuuza, ndiyo maana sitaki kurudi tena kwenye maisha yale.

Juma3tata:Unauzungumziaje mwenendo tasnia ya filamu za kibongo?

Calisah: Watu wengi wanasema wasanii wamekosa ubunifu, mimi sipendi kusema hivyo sababu ni kauli inayowavunja moyo wasanii wetu, tasnia ya filamu imekosa 'investors' (wawekezaji), mfano Bongo Fleva wasanii wake wanawekeza fedha nyingi ndo maana wanafanikiwa, nadhani wakipata wawekezaji wachache watafika mbali, nasapoti tasnia nzima na wasanii wake kama kina Ray , JB na wengine.

Juma3tata: Kitu gani kati ya simu, washkaji na Gym huwezi kuishi mbali nacho?

Calisah: Siwezi kuishi mbali na Gym kwa sababu ndiyo kitu kinachofanya niwe na mwonekano flani, kwa hiyo kupata kazi, wanawake na hela kunategemea mwonekano wangu wa mazoezi na siyo simu wala washkaji.

Juma3tata: Inajulikana uliwahi kuwa mapenzini na mrembo Wema Sepetu, kitu gani huwezi kukisahau kwenye uhusiano wenu?

Calisah: Kwanza Wema amenifanya niwe na 'comfidance', amefanya nione kila kitu kinawezekana, alinipa moyo wa kutafuta ili niendane na hadhi yangu, maana nilipomvaa yeye ilibidi maisha yangu yabadilike na amefanya nifahamike sehemu ambazo sikuwahi kufikiria kama nitafika, namshukuru na mpaka sasa tupo vizuri kama kaka na dada namheshimu sana.

Tukija kwenye tukio la ambalo siwezi kulisahau ni siku ya kwanza kwenda kulala kwa Wema, nililala na nilipoamka asubuhi tumbo la kuharisha likanikamata.

Unajua chumba cha Wema ni kikubwa harafu kina choo ndani, ishu ikaja napataje nafasi ya kwenda msalani mbaya zaidi kitanda kipo karibu na 'washroom' kwa hiyo chochote kikifanyika chooni aliyekuwa chumbani anasikia.

Ikabidi niombe maji ya kunywa ili akienda kuniletea mimi niingie chooni, akaenda kuchukua maji na kurudi fasta.

Nilikuwa naona aibu kumwomba niende chooni, baada ya kuona hataki kutoka na tumbo linazidi kuchafuka ikabidi nimwambie: Can i use your toilet, akaniruhusu ikabidi tu niingie nishushe mzigo, nikaangusha mzigo mkubwa kwa sauti, alisikia kila kitu maana chumbani kulikuwa kimya sana hakuna mtu anayeongea wala mbwa anayepiga kelele.

Baada ya kumaliza nikatoka zangu na tukio lile lilinisaidia kwa sababu alikuja kuniona ni mtu ambaye nipo 'real' si-fake maisha, alifurahi sana kutambua uwazi wangu kwake maana angekuwa mwingine angeficha ficha.

Juma3tata: Kwanini umeamua kufungua kampuni ya 0+Door Ltd na malengo yako ni nini?

Calisah: Kwenye tasnia ya mitindo hakuna wa kusema flani ni namba moja yaani amefanikiwa kijina na kiutajiri, tofauti na kwenye muziki unaweza ukajua msanii gani nii namba moja,mbili na tatu.., upande wa wanawake kwenye mitindo tunao kina Flaviana Matata, Happiness Magese, Genevieve na wengine, lengo langu ni kuwa 'agency' (Wakala) mkubwa wa kiume kwa hapa Tanzania kisha Kenya, Uganda na kwingineko ili mtu akitafuta google tu jina langu anajua mamodo freshi wanapatikana kwenye kampuni ya Calisah pekee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,437FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles