23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Bush kuzikiwa kwa heshima za taifa

WASHINGTONDC,Marekani



WIZARA  ya Ulinzi   imesema  maelezo zaidi juu ya mipango ya maziko ya Rais Mstaafu, George H. W. Bush, ambaye alifariki  dunia mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 94, yanaandaliwa na familia yake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi na wizara hiyo, Rais Bush ambaye alitumikia nafasi ya urais tangu mwaka 1989-1993, ataagwa kwa heshima zote za taifa kesho  katika Kanisa   Kuu la  Washington na kuzikwa Alhamisi katika makazi  yake   katika Jimbo la   Texas.

Ilieleza baada ya jana maandalizi hayo kuwa tayari, mwili wake ungewekwa katika ukumbi wa Rotunda ndani ya bunge la hapa  kwa ajili ya wananchi   kuuaga mpaka kesho  asubuhi, wakati utaratibu wa kupewa heshima zote za taifa uliondaliwa jana.

Tarifa hiyo ilieleza zaidi kwamba umma wa Wamarekani utaweza kuendelea kutoa heshima   za mwisho wakati mwili wa Rais Bush ukiwa katika jeneza kuanzia jana  saa 1:30  asubuhi     hadi Jumatano majira kama hayo.

Ikulu   ilitangaza juzi kuwa Rais Donald Trump  atahudhuria shughuli za kuuaga mwili wa wa kiongozi huyo.

Msemaji wa Ikulu, Sarah Sanders alisema  kesho  imepangwa kuwa siku ya  taifa ya maombolezi  na bendera ndani ya Ikulu tayari zimeshushwa nusu mlingoti kumuenzi kiongozi huyo.

Katika hatua nyingine, mbwa ambaye alikuwa akimuhudumia kiongozi huyo amepigwa picha akiwa amelala kando ya jeneza kama sehemu ya kutoa heshima zake za mwisho.

Mbwa huyo anayeitwa Sully, jana alitarajiwa kusafiri kwa ndege pamoja na jeneza lenye mwili huo kutoka mjini Texas hadi hapa ambako  ulitarajiwa kuanza kuagwa.

Picha iliyotumwa kwa njia ya mtandao wa Twitter na msemaji wa Rais  Bush, Jim McGrath,inamuonyesha  mbwa Sully akiwa kando ya jeneza ikiwa na ujumbe unaosema ‘Mipango imekamilika’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles