25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

BURUNDI YAJITOA ICC

BUJUMBURA, BURUNDI

TAIFA la Burundi imekuwa mwanachama wa kwanza wa Mahakama ya Kimataifa kuhusu uhalifu wa Jinai kujiondoa katika mahakama hiyo.

Serikali ya nchi hiyo iliuarifu Umoja wa Mataifa kuhusu hatua hiyo mwaka mmoja uliopita, na hii leo kujitoa kwao kunaanza kuidhinishwa rasmi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza limesema kuwa kujiondoa kwa Burundi ni masikitiko makubwa. Pia limesema ni kama kipimo cha jamii ya kimataifa kuhusu haki kwakuwa ni hatua sio ya kawaida.

Mahakama ya ICC imeanza kutathmini iwapo inaweza kuchunguza ghasia za kisiasa zilizoibuka baada ya rais Pierre Nkurunziza kuchukuwa madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula miwili katika katiba ya taifa hilo.

ICC bado ina uwezo kuchunguza uhalifu uliotekelezwa wakati Burundi ilipokuwa mwanachama wa mahakama hiyo. Lakini haiwezi kuchunguza uhalifu wowote wa siku zijazo.

Hatua hiyo inaweza kuwa mfano na kuonyesha viongozi wengine kwamba kujiondoa katika mahakama hiyo ni njia mojawapo ya kuepuka jicho la kimataifa hadi pale Jamii ya kimataifa itakapochukua hatua na taasisi kama vile Umoja wa Afrika ama baraza la usalama la umoja wa mataifa litakapowafuatilia washukiwa na kuyakumbusha mataifa kwamba kujiondoa katika ICC hakumaanishi moja kwa moja kwamba waathiriwa hawatopata haki.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles