25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

SANGA AUNDA KAMATI MPYA BODI YA LIGI

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

 

MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Clement Sanga, ameteua Kamati mpya ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi.

 

Wajumbe wanaounda kamati hiyo ambayo ataiongoza yeye mwenyewe ni Shani Mligo (Makamu Mwenyekiti), Boniface Wambura (Katibu), Issa Batenga, Leslie Liunda na Wakili Saleh Njaa.

 

Wengine ni Dk. Ellyson Maeja, George Malawa, Isaac Chanji, Baruan Muhuza, Mbakileki Mutahaba na Ally Mayay.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, kamati hiyo ya TPLB ndiyo inayoshughulikia uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na Ligi Daraja la Pili (SDL).

 

Pia Mwenyekiti ameteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi ya TPLB, ambao ni Kanali Charles Mbuge, ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Ruvu Shooting na Abuu Changawa (Majeki).

 

Kwa mujibu wa Ibara ya 28(vi) ya Kanuni za Uendeshaji za TPLB, Mwenyekiti ana nafasi ya kuteua wajumbe wawili kuingia kwenye Kamati ya Uongozi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles