28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Bulembo amvaa Edward Lowassa

abdallah-bulembo8Na Ruth Mnkeni, Dar es Salaam

MWENYEKITI Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, amemtaka aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowasa, kuwataja hadharani wafanyabiashara waliokuwa wanasaidia Ukawa kutozwa kodi kubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Bulembo alisema kauli ya Lowassa inalengo la kuigombanisha Serikali na wafanyabiashara, hivyo ni vyema akawataja hadharani ili kuondoa utata huo.

Alisema ni vema Lowassa amwache Rais Dk. John Magufuli, afanye kazi yake kwani ameshaonesha kwa vitendo umuhimu wa ulipaji kodi.

“Sisi tunamwomba Lowassa awataje hao wafanyabiashara au makampuni ambayo yalikuwa yanakisaidia chama chake na leo wanatozwa kodi kubwa, aweke wazi kabisa kwamba hapo awali walikuwa wanatozwa ngapi na sasa imeongezeka ngapi,”alisema.

Alisema kodi lazima itozwe kutokana na kwamba Serikali inategemea katika kujiendesha ambapo tayari matokeo ya ulipaji kodi yameshaonekana ikiwemo kutolewa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne.

“Leo hii ukienda hospitalini unapata huduma bora hakuna kulala chini, hizi ni jitihada za Rais Magufuli na ukweli ni kwamba huu ni utekelezaji wa ilani ya CCM,”alisema.

Alisema katika kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata elimu bora jumuiya hiyo ya wazazi ilitembelea zaidi ya shule 26 ambapo kati ya hizo 15 zilikuwa hoi.

“Hizi shule 15 tuliona zina matumizi mabaya ya fedha mfano shule ina wanafunzi 1000 lakini matumizi yake yanaonekana kwamba labda kila mwanafunzi anakula kilo mbili kwa siku, jambo ambalo changamoto na walimu wakuu watachukuliwa hatua za kisheria,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles