27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Bodi ya maji Bonde la pangani yatoa ufafanuzi rangi nyeusi mto Rau

Safina Sarwatt, Moshi

Bodi ya Maji Bonde la Pangani imetoa ufafanuzi kutokana na hali ya taharuki iliyotokea baada ya kuibuka kwa rangi nyeusi katika maji ya Mto Rau na kwamba athari hiyo imetokana na kuungua kwa mlima Kilimanjaro hivyo maji hayo hayana kemikali yoyote na ni salama.

Mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la mto Pangani, Segule Segule ametoa ufafanuzi huo leo Desemba 31, 2020 ofisini kwake mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akizungumza na wandishi wa habari.

Segule amesema baada ya kupata taarifa Desemba 16, 2020 wataalam walitembelea Mto Rau kubaini iwapo kuna uchafuzi huo unasababishwa na utiririshaji wa majitaka mtoni na kwamba Uchunguzi huo haukubaini utiririshaji wowote wa aina hiyo.

“Desemba 17,2020 tulitembelea upande wa chini, kati na juu ili kuchunguza kwa kina zaidi na kuchukua Sampuli za Maji katika maeneo hayo, Utafiti wa kimaabara wa sampuli hizo na kwamba utafiti umeonyesha hakuna kemikali yoyote bali majivu yalitokana na kuugua kwa mlima Kilimanjaro, “amesema Segule.

Amesema kuwa chanzo cha mto Rau unatokana na hifadhi ya mlima Kilimanjaro hivyo baada ya mvua kunyesha majivu hayo yalisafirishwa na maji na kuingia katika chanzo hiyo.

“Tumefuatilia ndani ya Msitu wa hifadhi ya Mlima Kilimanjaro tukishirikiana na wenzetu wa KINAPA ili kuangalia hali ya chanzo cha Mto Rau na kujua athari ikiyojitokeza inaanzia mahala gani hasa.

“Pia tumechunguza mito midogo midogo inayoingiza maji mto Rau kama vile Mto Mware na Mto Mrusunga na kwamba tumebaini kuwa maji ya mito hiyo hayajaathirika,”amesema

Amsema kuwa uchunguzi huo pia umefanyika katika mto Karanga ambao umeanza kuonyesha dalili ya maji kuwa rangi nyeusi athari ambayo imesababishwa na majivu baada ya kuungua kwa mlima.

“Kwa kuwa mvua zinazonyesha sasa ni katika maeneo hayo yaliyoungua upo uwezekano maji yanabeba majivu na kuyapeleka Mto Rau,” amesema.

Amesema Bodi ya maji bonde la mto pangani ndio wasimamizi wakuu wa Rasilimali za maji katika eneo la mikoa ya Kilimanjaro, Arusha , Tanga na Manyara (Wilaya ya Simanjiro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles