26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Harmonize awavuruga WCB akimsifia Diamond

KATIKA kuingia mwaka 2021, staa wa Bongo Fleva, Rajab Kahali ‘Harmonize’ amejikuta akiwavuruga mashabiki wa WCB baada ya kumwagia sifa bosi wake huyo wa zamani.

Na CHRISTOPHER MSEKENA

Harmonize ambaye yupo kikazi nchini Ghana, alitumia ukurasa wake wa Instagram kuposti picha ya Diamond na kuelezea jinsi ambavyo staa huyo alivumbua kipaji chake na kumfanya awe msanii nyota anayetegemewa Afrika Mashariki.

Konde Boy alimsihi Diamond akae peke yake ya kuutafakari ujumbe huo ambao anaamini ataona kitu kikubwa cha heshima alichokimaanisha katika posti hiyo.

Staa huyo wa singo Uno, anasema: “Asante kwa kubadilisha maisha yangu, pekee uliona dhahabu kwenye mchanga na giza jingi sana, leo hii Afrika nzima hasa Afrika Mashariki wanajivunia uwepo wangu, huu ni upendo wa milele, chochote ninachofanya najivunia wewe, mimi na mashabiki wa Konde Gang tunakupenda.”

Ujumbe huo ulipokewa vizuri na mastaa kibao wa ndani na nje ya Bongo ambao walimpongeza Harmonize kwa kumshukuru Diamond licha ya hivi karibuni kudaiwa kumponda vibaya Mondi kwenye goma lake jipya, Wapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles