26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

‘Nimejikuta Tuh’ ya Mozee Kamana, Gazuko yazua gumzo

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MWIMBAJI nyota wa Injili nchini, Mozee Kamana, amejikuta akiibua gumzo kwa mashabiki wa muziki huo punde baada ya kuachia wimbo wake, Nimejikuta Tuh aliomshirikisha Gazuko Junior.

Ndani ya wimbo huo wawili hao wamerap kwa kupokezana ambapo Mozee amevaa uhusika wa mlevi aliyepotea njia na kujikuta ameingia kanisani mbele ya mchungaji Gazuko ambaye anafanikiwa kumwombea na kumvuta kwa Yesu.

Akizungumzia wimbo, Nimejikuta Tuh, ambao tayari unapatikana katika mitandao yote ya kusikiliza muziki duniani, Mozee anayemiliki wa studio za Lokhano Music alisema anamshukuru Mungu kwa kumpa mawazo tofauti yanayozua gumzo kwaajili ya kuujenga Ufalme wa Mbinguni.

“Wimbo umepokewa vizuri, tumeachia audio na Mungu akijaalia muda wowote tunaweza kutoa video, kikubwa ni sapoti ili huduma yangu izidi kukua na kuwafikia watu wengi,” alisema Mozee ambaye ni mshindi wa Wimbo Bora 2020 katika tuzo za Moro Inspiration Awards.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,621FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles