31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Bodi ya Ligi yaituliza Azam

 WINFRIDA MTOI -DAR ES SALAAM 

BODI ya Ligi (TPLB) imeituliza Azam FC iliyotarajia kuanza mazoezi Jumatano ya wiki hii kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara. 

Kikosi hicho kilikuwa kiingie kambini baada ya Serikali kutangaza rasmi tarehe ya kurudi tena ligi iliyokuwa imesimamishwa kutokana na janga la ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona. 

Akizungumza na MTANZANIA, Mkuu wa Kitengo cha Habara na Mawasiliano Azam FC, Thabith Zakaria ‘Zaka Za Kazi’, alisema japo waliwataarifu wachezaji wao kuwa wanaanza mazoezi Jumatano, hilo sasa halitawezekana. 

Alisema sababu ya kusitisha mazoezi ni baada ya Bodi ya Ligi kuwaambia wasianze hadi pale watakapopewa muongozo. 

“Mazoezi tulitaka kuanza Jumatano, tumesitisha kwa sababu Bodi ya Ligi wametuambia hadi watakapotoa mwongozo, hivyo tunawasubiri,” alisema Zaka Za Kazi. 

Alisema wanachokifanya kwasasa ni kufuatalia taratibu za kuwasafirisha wachezaji wao waliopo nje ya nchi pamoja na makocha. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,612FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles