26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

BOBI WINE AZUNGUMZIA MATESO ALIYOPITIA UGANDA

KAMPALA, UGANDA

MWANAMUZIKI maarufu nchini Uganda ambaye ni Mbunge, Bobi Wine ameeleza katika ukurasa wake wa Facebook namna kikundi cha watu kilivyomtesa alipokuwa kizuizini.

Mbunge huyo kutoka kambi ya upinzani, ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi anakabiliwa na mashtaka akidaiwa kurushia mawe gari la rais lililokuwa kwenye msafara wa Rais Yoweri Museveni mwezi uliopita.

Alikamatwa August 13 na kuachiliwa wiki iliyopita na kwa sasa yuko Marekani kwa matibabu zaidi kufuatia mateso aliyoyapata.

Jeshi nchini Uganda limekana tuhuma dhidi yake na kuita kuwa ni upuuzi huku Rais Museveni akiziita taarifa za vyombo vya habari nchini mwake kuwa ni habari bandia.

Bobi Wine ameamua kuandika kuweka sawa kilichomsibu kutokana na kile alichosema Rais Museveni na maofisa wa serikali yake wamekuwa wakieleza tofauti na ukweli juu ya kilichotokea katika mji wa kaskazini-magharibi mwa Arua.

“Walinipiga, walinipiga na kunipiga kwa buti zao, hakuna sehemu ya mwili wangu ambayo haikuguswa na kipigo chao. Sehemu hizo ni pamoja na macho, pua na mdomo wangu. Wakapiga viwiko vya mikono yangu na magoti yangu, watu wale hawana utu hata kidogo.

“Walizivuta sehemu zangu za siri na kuminya kende zangu huku wakiendeleza kipigo kwa kutumia vitu vingine, wakaanza kupiga vidole vyangu kwa kutumia kitako cha bastola. Nilikuwa katika maumivu ya ajabu,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles