29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Blatter amfuta kazi bosi Fifa

Press-Conference-at-FIFA-headquartersZURICH, USWISI
MKURUGENZI wa Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Walter De Gregorio, amefutwa kazi baada ya kutoa maneno yenye utani kuhusu shirikisho hilo kwenye televisheni ya Uswisi.
Gregorio alizungumza kwenye kipindi cha Schawinski kuwa: “Rais wa Fifa, Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mawasiliano wote wanasafiri kwenye gari. Nani ni dereva? Jibu ni polisi.”
Fifa imetangaza jana kwenye taarifa yao kuwa De Gregorio ameamua “kuachia madaraka kwenye ofisi yake”.
Lakini inaaminika ya kuwa aliambiwa ajiuzulu na Rais wa Fifa, Sepp Blatter na katika taarifa hiyo imeeleza kuwa De Gregorio atabakia Fifa kama mshauri hadi mwishoni mwa mwaka huu.
Blatter yeye alitangaza ataachia ngazi kuongoza taasisi hiyo mwanzoni mwa mwezi huu kutokana na kashfa kubwa ya rushwa inayoiandama Fifa na sasa uchaguzi mwingine utafanyika kati ya Desemba na Februari mwakani.
De Gregorio, 50, amedumu kwenye wadhifa huo tangu Septemba, 2011 na amekuwa mtu wa karibu sana wa Blatter tangu achukue majukumu hayo na inaelezwa Blatter hakufurahishwa na maneno yake hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles