27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Calum Chambers aiponza Arsenal

LONDON, ENGLAND
TIMU ya Arsenal imefunguliwa mashtaka na Chama cha Soka England (FA) kwa madai ya kuwa walikiuka sheria za uwakala wa soka walipomsajili beki Calum Chambers kutoka Southampton Julai mwaka jana.
Wakala Alan Middleton naye pia amefunguliwa mashtaka kwa kukiuka sheria za usajili na ametakiwa kujibu madai hayo hadi kufikia Juni 17 mwaka huu, Arsenal imetakiwa nayo kujibu Juni 26 baada ya kuombwa kufanya hivyo mara kadhaa.

Chambers, 20, aliyejiunga na Gunners kwa kitita cha pauni milioni 16, amefanikiwa kucheza mechi 36 msimu uliopita na kuisaidia timu hiyo kushika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu England (EPL).
Chambers yumo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya England chini ya miaka 21 kinachojiandaa na michuano ya Ulaya inayotarajia kutimua vumbi Jamhuri ya Czech Jumatano ijayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles