26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Blac Chyna, Rob watarajia mtoto wa kike

Blac Chyna
Blac Chyna

NEW YORK, MAREKANI

KAKA wa Kim Kardashian, Rob Kardashian na mpenzi wake Blac Chyna, wameweka wazi kuwa wanatarajia kupata mtoto wa kike Oktoba, mwaka huu.

Awali wawili hao walisema ujauzito wa Blac ni wa mtoto wa kiume, lakini kumbe alikuwa hajafanya vipimo, ila wiki hii wamefanya vipimo hivyo na kugundua kuwa watapata mtoto wa kike.

Kupitia akaunti ya Twitter, Blac ameonesha kuwa na furaha kubwa baada ya kupokea taarifa hizo za mtoto wa kike.

“Familia yangu inatarajia kukua ifikapo mwezi Oktoba, natarajia kupata mrembo tofauti na awali ambapo habari zilienea kuwa nitapata mtoto wa kiume,” aliandika Blac.

Hata hivyo inadaiwa kuwa Rob anaonesha kukosa furaha baada ya kuambiwa kuwa ni mtoto wa kike, inaonesha kuwa Rob alijiandaa zaidi kupata mtoto wa kiume.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles