24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Bima ya mazao kuanza na wakulima wa pamba, kahawa

Derick Milton – Simiyu

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imezindua rasmi mpango wa Bima ya mazao mbalimbali ambao utaanza na wakulima wa zao la pamba Mkoa wa Simiyu na kahawa katika Mkoa wa Kagera.

Mpango huo umezunduliwa leo na Waziri wa kilimo Japhet Hasunga katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu yanakoendelea maonyesho ya sikuu ya wakulima kitaifa (Nanenane).

Akizungumzia bima hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima ya Taifa (NIC), Dk. Elirehema Doriye, amesema wakiwa kama watekelezaji wa mpango huo watahakikisha wakulima wote nchini wanapatiwa bima ya mazao yao.

“Kwa hatua za mwanzo tutaanza na wakulima wa pamba na kahawa, kisha tutaenda kwa wakulima wengine wote nchi nzima, bima hii itamsaidia mkulima wa chini kuendelea na shughuli za kilimo hata kama atapata majanga ya mazao yake kushambuliwa na magonjwa, wanyama, ukame na mvua iliyozidi,” amesema Dk. Doriye.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, ameitaka NIC kuhakikisha wakulima wote wa mazao makuu matano wanajiunga na bima hiyo ili kuweza kubadilisha kilimo kuwa cha kisasa zaidi na chenye tija.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles