23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Watoto milioni tatu wakabiliwa na utapiamlo

Amina Omari – Tanga

Takribani watoto milioni tatu wenye umri chini ya miaka mitano nchini wanakabiliwa na ugonjwa wa utapiamlo uliokithiri .

Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wa mkakati wa udhibiti wa mbu na wadudu dhurifu katika Halimashauri ya Jiji la Tanga.

Amesema kuwa kutokana na ukubwa wa tatizo hilo wizara ya Afya inatarajia kuja na mpango mkakati wa kudhibiti tatizo hilo kwa watoto nchini.

“Kuanzia mwaka ujao wa fedha Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Tamisemi tutakuja na mpango wa Kinga ili kuhakikisha tunapunguza na kudhibiti magonjwa yanayoweza kuzuilika “amesema.

Aidha amesema kwa Sasa Wizara za Afya na ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi), inatarajia kuja na mpango mkakati wa kuhakikisha inaboresha huduma za Kinga na tiba ili kuweza kupunguza magonjwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za afya kutoka Tamisemi, Dk Ntuli Kapologwe, ameziagiza Halimashauri nchini kutenga fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya mbu pamoja na wadudu waenezao magonjwa mbalimbali.

Amesema kwa sasa nchi inaelekea kwenye uchumi wa Kati hivyo ni jukumu la serikali kuhakikisha wananchi wanakuwa huru na magonjwa yanayoenezwa na mazalia ya wadudu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles