Ummy: Tunaendelea kutekeleza mpango wa kudhibiti wadudu dhurifu

0
648
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu

Amina Omari – Tanga

Serikali imesema itaendelea kutekeleza Mpango kabambe wa Taifa wa kudhibiti Mbu na wadudu dhurifu nchini ili kudhibiti magonjwa kama malaria, Dengue, homa ya manjano, matende na mabusha kwa kununua madawa na vifaa vya kupulizia dawa za kuua mbu pamoja wadudu wanaozambaza magonjwa hayo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, wakati wa Uzinduzi wa uhamasishaji wa mkakati wa udhibiti wa mbu na wadudu dhurifu katika Halimashauri ya Jiji la Tanga.

Amesema kuwa ili kuimarisha kampeni ya kutokomeza mbu nchini, Wizara imeipatia Halmashauri ya Jiji la Tanga mashine kubwa ya kisasa (Fogging Machine) ya kupuliza dawa ili kuuwa mbu wapevu na wadudu dhurifu.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Wizara itaendelea kubuni mikakati mingine zaidi na kutafuta rasilimali fedha ili kutokomeza mbu na wadudu dhurifu nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here