23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Bil/ 700 kutatua changamoto ya maji Kanda ya Ziwa

Mwandishi Wetu, Mwanza

Serikali imewekeza Sh bilioni 788 kwenye miradi ya maji mikoa ya Kanda ya Ziwa ili kutatua changamoto hiyo mkoani humo.

Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amewataka wananchi kuendelea kuiamini serikali kwani imewekeza fedha nyingi kutatua changamoto ya maji nchi nzima.

Profesa Mkumbo amesema kwa sasa serikali ipo katika hatua za mwisho kwenye mazungumzo na Benki ya Ulaya (EIB) kupokea kiasi cha Sh bilioni 80 kwa lengo la kumalizia mradi wa maji eneo la Usagara wilayani Misungwi na miradi mingine midogo.

“Serikai hii ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, inatambua tatizo la maji walilokuwa nalo wananchi hivyo basi inajitahidi kuhakikisha kwamba mpago mkakati huu wa miaka ishirini wa miundo mbinu unatekekelezwa kwa uweledi,” anesema Profesa Mkumbo.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira, Mwauwsa, Mhandisi Antony Sanga, amesema lengo la kuongeza bei au mabadiliko hayo ni pamoja na kujenga miradi mipya yenye kuongeza mtandao wa usambazaji maji ili kuyafikia maeneo yanayokosa maji na yanayopata maji kidogo pammja na kutanua mfumo wa uondoshaji majitaka kwenye maeneo ambayo hayana mfumo huo.

“Pamoja na huduma nyingine, pia tunafanya matengenezo na ukarabati wa mambomba ya wateja yanayosababisha mivujo ya maji bila kuwatoza gharama za matengenezo na ukarabati,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles