28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Jafo apigilia msumari sakata la watumishi Simiyu kulipishwa mashine ya Ultrasound iliyoibwa

Mwandishi Wetu

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jafo mepigilia msumari sakata la watumishi wa Hospitali ya Mji wa Bariadi wasichangishwe fedha kufidia mashine ya Ultrasound iliyoibwa hospitalini hapo.

Jafo ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 15, kauli ambayo inamuunga mkono Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini ya kutaka watumishi hao wasilipishwe fedha kama walioamriwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga jana Jumatano Agosti 14.

Pamoja na mambo mengine, Jafo amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka kuunda tume ya uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na wizi wa mashine hiyo.

“Kulikuwa na maelekezo kuwa wale watumishi 137 walipie ile mashine kwa kukatwa kwenye mshahara yao, nielekeze kwamba watumishi wetu hawa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana, na tukumbuke hata tulipopata janga pale Morogoro watumishi wetu wa idara ya afya muda mwingi ndiyo walikuwa kimbilio kuwasaidia wananchi.

“Kitendo kama hiki ni kuwakatisha tamaa na kuwaweka katika ya sintofahamu lakini kumbe inawezekana kuna watu walihusika. Lengo hapa ni kuwatafuta waliohusika, wabainishwe ni kina nani wachukuliwe hatua lakini pia wahakikishe mashine hii inarudi.

“Kwa hiyo nitoe maelekezo kuwa watumishi hawa wasichangishwe fedha ya aina yoyote kwa sababu siyo jukumu lao, ni jukumu la ulinzi kwa hiyo Mkuu wa Mkoa namuelekeza kwanza aunde tume ya uchunguzi kuwabaini wahusika na watumishi hao waachwebwafanye kazi kwa sababu tunawategemea sana haipaswi kuwabebesha mzigo usiowahusu,” amesema Jafo.

Mashine hiyo iliibiwa hospitalini hapo Agosti 5, mwaka huu ambapo jama mkuu wa wilaya alitoa agizo kwa watumishi hao kuchangia kulingana na mishahara yao ili kufidia mashine hiyo jambo lililopingwa na Sagini ambaye leo mchana alitangaza kutengua agizo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles